Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi Jumuiya za Umoja wa Afrika ili kuendeleza utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi wanachama.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani 2021 yaliyofanyika Jijini Abidjan nchini Côte d' Ivoire  leo.

 “Lengo kuu la kushiriki katika Maadhimisho haya ni kujifunza  na kuangalia namna ya kendeleza utalii wetu hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na janga Uviko 19 lililoikumba dunia”amesisitiza Mhe.  Masanja.

Aidha, Mhe. Mary Masanja ameongeza kuwa ushiriki huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na pia kuvitangaza vivutio vya Utalii vilivyoko nchini Tanzania ikiwa ni moja ya juhudi za kuunga mkono kazi anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii duniani.

Kauli mbiu ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka huu ni “Utalii kwa Maendeleo Shirikishi/ Jumuishi”







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...