Na Avila Kakingo, Globu y jamii
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakuu wa Mikoa yote hapa nchini kuchukua hatua zinazositahiki za kuwapanga wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga kuwapanga vyema bila kuleta vurugu, fujo na uonevu.

Ameyasema hayo leo Septemba13, 2021 mara baada ya kuwaapisha wabunge wateule na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Ikulu ya jiji Dodoma. Amesema kuwa wamachinga hawalipi kodi lakini mwenye duka anatakiwa kulipa kodi kitendo cha wamachinga kukukaa mbele ya maduka kinakosesa serikali kupata mapato yake.

“Watu hawa wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo tofauti tofauti, wakuu wa mikoa wanawapanga, wakuu wa wilaya wanawapanga lakini kumekuwa na Luxicity watu wamepumzika, kiasi ambacho watu hawa wameenea kila mahali mpaka kwenye maduka, wao wanaziba maduka hayauzi wao wanauza mbele, mpaka sasa wenye maduka baadhi yao wamepata mtindo wa kutoa bidhaa ndani na kuwapa wamachinga kuuza kwa sababu watu hawaingii ndani lakini tendo hili linatukosesha kodi kwa sababu Machinga halipi kodi lakini mwenye duka anatakiwa kulipa kodi.”

“Kwahiyo wito wangu kupitia jukwaa hili ingawa hapa si mahali pake, kwa wakuu wa Mikoa, kuchukua hatua za kuwapanga vyema na ninaposema kuchukua hatua za kuwapanga vyema, sitaki kuona yale ninayoyaona kwenye Tv, Ngumi Kupigana kufukuzana, kuchafuliana,vitu kumwagwa aaaha…” Amesema Rais Samia

Amesema kuwa wanaweza kuchukua hatua vizuri na kuwapanga vyema bila kuudhi wenye maduka na wamachinga na maisha yakaendelea.

Hata hivyo Rais Samia amewaasa wamachinga kufuata sharia na kanuni zilizopo, lakini wajitahidi kufuata yale wanayopangiwa na wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya.

Licha ya hayo Rais Samia amesema kuwa Serikali imetoa imetoa fursa kubwa kwa wamachinga kufanya biashara zao kama njia ya ajira kwao na kujipatia mkate wa kila siku kwani serikali inapungukiwa na mzigo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...