Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako (katikati) akikagua baadhi ya vifaa vinavyotumika kujenga Shule ya Sekondari ya Mfano jijini Dodoma.Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma, Luteni Kanali Philemon Komanya akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa Shule hiyo.
Mafundi kutoka Kampuni ya Suma JKT ambao wanatekeleza ujenzi wa mradi wa Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma wakiendelea na kazi ya ujenzi huo.
Muoenkano wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma ambayo inajengwa na Kampuni ya Suma JKT.
Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imetoa onyo kwa wasimamizi wa mitihani na walimu Nchini kuacha tabia ya udanganyifu wa mitihani huku ikiahidi kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika kuvujisha mitihani ya Darasa la Saba itakayoanza Septemba 8 na 9 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako leo jijini Dodoma wakati alipoenda kukagua Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa katika eneo la Iyumbu.
Amesema katika miaka miwili iliopita kumekuwa na tabia ya udanganyifu kwa wasimamizi wa mitihani ya Taifa katika shule mbalimbali hivyo serikali inatoa onyo kwa wasimamizi wenye tabia hiyo kwa sababu wamejianda kuhakikisha watu hao wanabainika na kuchukuliwa hatua kali.
" Naomba wasimamizi wote mfanye kazi ya usimamizi kwa weledi ili wanafunzi watahiniwa wafanye mitihani sahihi kwa kutumia akili zao na uwezo waliofundishwa darasani,” Amesema Prof Ndalichako.
Prof Ndalichako pia ameitaka Kampuni ya ujenzi ya Suma JKT inayojenga shule hiyo ya mfano kukamilisha ujenzi wa madarasa kabla ya Februari mwakani kama mkataba unavyoelekeza ili wanafunzi waanze kuitumia.
Amesema shule hiyo imetumia Sh Bilioni 17 kwa ajili ya ujenzi huo ambayo mwakani inahitajika kuanza kutumika na wanafunzi ambao watachaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka ujao wa masomo.
Ameongeza uliokuwa ukifanyiwa kazi kwa muda mrefu wa kuimarisha elimu ya sekondari ambapo alisema mradi huo tayari umekwishaanza na fedha zimetolewa kiasi cha Dola la Kimarekani Milioni 74 ambazo ni sawa na Bilioni 170 za kitanzania.
Amesema fedha hizo tayari zimekwishapangiwa matumizi na moja ya matumizi ni kwenda kujenga shule za sekondari kwa ajili ya wasichana
ambazo ni za bweni na kwa kuanzia wataanza na Mikoa 10 na kila shule itatumia kiasi cha Sh Bilioni nne.
Amesema pia kutakua na ujenzi wa Shule za Kata za Sekondari katika Halmashauri 184 ambazo zitajengwa katika Mikoa 10 Nchi nzima na Mikoa hiyo itatangazwa na Tamisemi.
Naye msimaizi wa ujenzi wa mradi wa shule hiyo Luteni Kanali Philemon Komanya amesema ujenzi wa shule hiyo umefikia asilimia 60, ambapo ameahidi kutekeleza ombi la Waziri Profesa.Ndalichako la kuhakikisha shule hiyo inakamilika kabla ya Februari 2022 ili wanafunzi wanaohitimu waweze kuanza kusoma hapo mwakani.
" Tumepokea maelekezo ya Serikali kupitia Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Ndalichako ya kuhakikisha tunatimiza masharti ya mkataba wa ujenzi kwa kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.
Sisi kama Jeshi tunatekeleza ujenzi huu kwa kufanya kazi usiku na mchana na kama Waziri Prof Ndalichako alivyotuomba kama tunaweza kukamilisha kabla ya muda uliopangwa tumhakikishie kuwa tutateleleza ombi lake hilo," Amesema Luteni Kanali Komanya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...