SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeruhusu mchezo huo kuingia mashabiki wasiozidi 10,000.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo kutoka CAF wakiruhusiwa kuingiza namba hiyo ya mashabiki katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.
"Tumepokea majibu ya ombi letu la mashabiki kuingia uwanjani ambapo CAF wameturuhusu kuingiza mashabiki 10,000 tu katika mchezo huo," alisema Ndimbo.
TFF wametangaza viingilio vya mchezo huo huku kima cha chini kikiwa ni shilingi elf 3,000 kwa mzunguko na VIP B&C 5,000.
Stars itakuwa wenyeji katika mchezo wake wa tatu wa kundi J ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Qatar mwakani, utakaochezwa katika Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.
Kuelekea mchezo huo, Taifa Stars inaongoza kundi hilo baada ya kushinda mechi moja dhidi ya Madagascar na kutoka sare ilipocheza ugenini dhidi ya DR Congo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...