Raisa Said, Lushoto.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro amewataka Wazazi na Walezi kutokuwaacha vijana wao nyumbani wanapomaliza elimu ya msingi na sekondari na badala yake wawaendeleze kielimu ili waweze kubobea kitaaluma katika karne hii ya Sayansi na teknorojia .
Pia amewataka Wazazi hao kuacha mara moja tabia yakuwarubuni Watoto wao kufanya vibaya katika mitihani yao ya kitaifa kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani [UYAYA} ili wao wajipatie kipato.
Wito huo ameutoa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mbwei wilayani humo ambako kwa miaka mitatu mfululizo shule tatu za msingi zilizopo katika kata hiyo zimeshika nafasi ya mwisho katika mitihani ya kumaliza darasa la Saba.
"Sasa hivi kuna janga la corona lakini Katika kata hii kunajanga la kuferi hii ni aibu kubwa tubadilike tusiwarubuni watoto wetu kufanya vibaya mitihani yao ili wakafanye uyaya Mombasa,Tanga,Dar Es Salaam na Arusha" Alisema Mkuu hiyo wa Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa watoto ni taifa la kesho hivyo wanatakiwa kujengewa mazingira mazuri ili waweze kutimiza ndoto zao za badae badala ya kuruhusu kwenda kufanya kazi za ndani kwa watu.
"Ndugu zangu hamkuzaa ili watoto wenu waende kufanya kazi za ndani kwa watu acheni mara moja tabia hiyo ya kuwaambia watoto wafanye vibaya mitihani yao kabla hatua Kali zakisheria hajizachukuliwa kwa wazazi wote watakaobainika kufanya hivyo" Alisisitiza
Aliongeza kuwa inasikitisha Sana kuona watoto wanafeli lakini shule zinashika nafasi ya mwisho hii ni aibu kubwa na haikubaliki Katika Wilaya hii,alitolea mfano kwa mwaka 2019 shule ya msingi Mbwei Wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 142 na waliofauli walikuwa tisa na kwa mwaka 2020 waliofanya mtihani walikuwa 91 waliofauli ni wanne .
Kwa upande wa shule ya Mavului kwa mwaka jana walifanya mtihani walikuwa 45 waliofauli kwenda sekondari walikuwa wa wili na kwa shule ya Mhezi kwa walifanya mtihani mwak jana walifanya mtihani walikuwa 95 waliofaulu walikuwa tisa.
Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza kuwa enzi za kufelisha zilishapitwa na wakati" Mimi nimemaliza elimu ya msingi mwaka 1990 tukafaulu watu watano wengine walikosa shule sababu hakukuwa na shule za kata lakini hivi Sasa shule zipo nyingi hivyo mnatakiwa mfaulishe watoto wengi Kwakuwa shule zipo na Rais anatopesa kila shule ambapo kila shule inapata laki tano kwa mwezi na kwa mwaka milion sita" Alisisiza Lazaro.
Lazaro alisema kuwa Rais Samia kila mwezi amekuwa akitoa sh.Laki tano kila shule ili watoto wasichangishwe wapewe elimu bure ambapo kila shule kwa mwaka inapewa mili.sita.
Pia alitumia fursa hiyo kuwahimiza Wazazi kuchangia chakula shuleni sababu chakula kinaongeza ufaulu
Nae Mbunge wa Jimbo hilo Shabani Shekilindi Maarufu Bosnia alisema kwa miaka mitatu mfululizo shule hizo zinaferisha lakini walifanya utafiti wakagundua Kuna wazazi wanawarubuni watoto wao wafanye vibaya mitihani yao sababu walimu wanadai watoto darasani wako vizuri lakini kwenye mitihani yao ya kumaliza elimu yao ya msingi ndo wanafanya vibaya.
Shekilindi alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamewafanya watoto wao kitega uchumi sababu kila mwezi watoto waliopo mijini kufanya kazi za ndani uyaya huwa wanawatumia wazazi wao shilingi elfu 20 hadi 30 baad ya kupewa mshahara yao kila mwezi.
Zitta Thomas ni Mwalimu Mkuu Shule ya msingi Mbwei alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni mlundikano wa Wanafunzi katika darasa moja hivyo ametupa kilio chake kwa serikali kuona umuhimu was kuongeza shule nyingine ili kuwapa nafasi walimu kufundisha kwa weledi na Wanafunzi kuelewa kwa ufasaha.
Mwalimu huyo pia alisema muamko mdogo wa elimu Katika kata hiyo ni sababu Kuna wazazi hawaelewi umuhimu wa elimu hivyo ameiomba serikali itunge sheria za kukomesha tabia ili kuwa nusuru watoto wanamaliza elimu yao .
Nuru Mdimu ni Mzazi na Mkazi wa kata Mbwei alisema sio kweli kwamba wanawarubuni watoto woa kufanya vibaya katika mitihani yao nakwamba yeye changamoto kubwa anayoiona inasabaisha watoto kufanya vibaya ni wingi was wanafunziuliopo Katika shule hizo.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lushoto Emanueli Vuli alisema kutokana na changamoto hiyo wameanza mikakati kwaajili ya kuongeza ufaulu kwa kuongeza walimu pamoja na kuanza mkakati wa kugawanya shule hiyo lengo kuboresha elimu Katika kata hiyo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...