Raisa Said,Muheza
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo amesema Wilaya hiyo imetengewa kiasi cha fedha sh.1.5 Bilioni za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Hayo aliyasema wakati Akizungumza na Wananchi wa Tarafa ya Bwembela Wilayani humo ambapo alisema Fedha hizo ni sehemu ya 1.3 trilion zilizotolewa na serikali hivi karibuni.
Mkuu huyo wa Wilaya Bulembo alisema fedha hizo walizotengewa zinakwenda kumaliza changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madarasa, bweni na madarasa 10 ya shule Shikizi na hivyo kufanya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha Kwanza na wale wa Shule shikizi kuondokana na changamoto hiyo.
"Tunaishukuru Serikali ya Rais Mama Samia kwa kutupatia wana Muheza fedha hizo. kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa 57, ujenzi wa vituo vitatu vya shule shikizi vyenye madarasa 10, ujenzi bweni moja la Wanafunzi wenye mahitaji maalum, na ujezi wa vyumba vya huduma za wagonjwa mahututi ( ICU) " Alisema Bulembo.
Akitoa mchanganuo wa fedha alisema kwenye ujenzi wa ICU wametengewa sh milion 100 huku bweni la Wanafunzi wenye mahitaji maalum likitengewa sh.milion 80.
Kwenye Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imepatiwa Vyumba 57 vya Madarasa kwa shilingi Milion 20 kwa chumba kimoja hivyo kufikia . 1.1 bilion
katika vyumba vya madarasa vitakavyojengwa katika vituo shikizi vimetengewa sh.miion 200,000,000
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...