Na Khadija Kalili, Kibaha
MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani kuacha tabia ya kuwa na makundi ndani ya chama kwani ni adui mkubwa kuwa wanasiasa wanaoishi kwa visasi na kutosameheana kabla na baada ya uchaguzi huku akiwasisitiza kuachana na siasa za makundi kwani hazina tija ndani ya chama.
Makamu wa Rais amesema hayo leo Kibaha alipokua katika ziara ya kujitambulisha kama mlezi wa Mkoa wa Pwani ambapo pia pia yeye ni mjumbe wa kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Tukasemane kwenye vikao vyetu tukatafute suluhisho tukiwa ndani ya vikao na tukitoka nje wote tuwe tumeridhiana pia tunapokwama tuwaite wazee Ili waweze kutupa busara zao za kukabiliana kutoelewana miongoni mweru mimi binafsi inapobidi niiteni wakati wowote nipatieni taarifa endapo kuna migogoro
ndani ya chama nasema hivi sababu migogoro ni kansa mbaya sana" alisema Dkt. Philip Mpango.

Dkt. Mpango aliongeza kwa kusema viongozi wanatakiwa kuwa na mahusiano mazuri wanachama pamoja na serikali yao Ili chama kiendelee na kuwa imara lazima kuwe na mahusiano mazuri chama chetu kina kanuni zake za kujiendesha tuzisimamie ipasavyo.

Wakati huohuo amewaambia Wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa wa Pwani kumpa ushirikiano Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge aliyemtaja kuwa ni Kamisaa na Kada wa CCM ambaye anamfahamu kwa miaka mingi wampe ushirikiano wa kutosha Ili kwa pamoja waweze kukijenga chama.

Ameishukuru kamati yote ya siasa ya Mkoa kwa mapokezi mazuri na kwa wanachama wote waliojitokeza na kumsikiliza.

Alisema kazi iliyopo mbele ya viongozi wa siasa ni kusimamia yale yote ambayo waliayaahidi ili wale wananchi ambao tuliwaahidi na wakatupigia kwani uchaguzi ujao hauko mbali.

Pia amewataka vijana wakachanje chanjo ya Uviko 19 Ili waweze kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao hata yeye ulimpata mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani (RC) Abubakari Kunenge akizungumzia kuhusu ziara hiyo amesema kuwa lengo ni kuboresha mambo mbalimbali ya kiserikali ikiwemo kukagua miradi sababu serikali inatekeleza ilani ya chama na ilani ya chama ni ahadi ambazo viongozi wetu walitoa ahadi mbalimbali na sisi ni watekelezaji.

"Tuimarishe umoja na ushirikiano miongoni mwetu ndani ya chama ,tutekeleze maagizo yote kutoka kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...