Raisa Said,Kilindi

IDARA ya Afya Wilayani Kilindi Mkoani Tanga imesisitiza umuhimu wa kunyonyesha mtoto maziwa ya mama,kwani yanamsaidia mtoto kupata lishe bora na humsaidia kukabiliana na maradhi mbalimbali likiwemo tatizo la udumavu na Ukondefu

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chochole amesema jamii ikitambua umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa ya mama hasa katika kipindi cha miezi sita inasaidia mtoto kumjenga mwili wake kuwa na lishe bora,kwani bila kufanya hivyo mtoto anaishi akiwa na afya isiyoimara kwa kusumbuliwa na magonjwa mbalimbali .

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Mwandishi wa Habari hizi wamesema pamoja na elimu inayotolewa na serikali kuhusiana na suala la unyonyeshaji watoto maziwa ya mama,baadhi baadhi ya wazazi wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kutimiza majukumu yao ya unyonyeshaji.

Amina Omary mkazi wa Songe alisema baadhi ya wanawake hasa wanaopewa mimba na wanaume na kutekelekezwa wanashindwa kunyonyesha watoto ipasavyo kutokana kujikuta wakisongwa na majukumu ya utafutaji na wengine kukosa chakula na hivyo kutokuwa na maziwa ya kutosha

‘‘Mimi nnapojifungua huwa nahakikisha namnyonyesha mtoto miaka miwili na watoto wangu huwa na afya nzuri" Alisema Mama huyo mwenye watoto watatu

Mwanamkasi Mbwana  alisema kuna tatizo la wanawake kutonyonyesha ipasavyo ilihali wananyonywa na wanaume kila siku.

‘‘Kuna wanawake kila siku wananyonywa na waume zao,kwanini wasiwanyonyeshe watoto ili kuwajengea uwezo katika makuzi yao.Serikali iendelee kutoa elimu kwenye mikutano na hata wanaohudhulia kliniki‘alisema Mbwana

Kwa upande wake Mratibu wa lishe  wilayani  Fikiri Adamu humo alisema hivi karibuni kwenye  Maadhimisho hayo wametoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu ya unyonyeshaji maziwa ya mama kwa mtoto,na kwamba elimu huwa inatolewa kila siku kwa wanawake wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya kujifungua.

Mratibu  huyo wa lishe aliongeza kwa kutoa wito kwa jamii ,wanawake kuzingatia suala zima la unyonyeshaji ili  kuwakinga watoto na magonjwa mbalimbali yanayotokana na kukosa lishe bora.

Alisema Maziwa ya mama hasa mara baada ya kujifungua huwa ni lishe bora kwa mtoto ,huku akiwaonya wanawake ambao huyakamua maziwa hayo kwa madai kuwa ni machafu jambo ambalo ni kumpunguzia mtoto lishe bora.

Mganga Mkuu Wilayani Kilindi DK Daniel Chochole

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...