Mfuko wa Amne Salim umechangia kiasi hicho ili kusaidia katika tafiti zinazofanywa na Watafiti kutoka MUHAS kupitia ugonjwa wa Uviko 19.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS Prof Andrea Pembe amesema Wanafurahi kuungana na mfuko wa Amne Salim ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu wa Zamani Dkt Salim Ahmed Salim utakaowawezesha wataalam kufanya tafiti kuhusu ugonjwa Uviko 19.
Prof Pembea amesema, Hatua hiyo ilyofanywa na Mfuko wa Amne Salim utahamasisha watu weng wenye nia njema kuunga mkono tafiti za Uviko 19 zinazofanywa na Chuo cha MUHAS.
“Hii itasaidia watafiti wachanga na wanaoibuka kufanya tafiti zao ambazo zinakuja kuleta majibu chanya kwa jamii na kutambua namna ya kupambana na magonjwq,”amesema
“Tafiti hizi zitasaidia ushindani na uwajibikaji ndani ya Taasisi katika kuelewa,kujilinda, kupambana na athari za ugonjwa wa Uviko 19,”
Prof Pembe amesema, ugonjwa wa Uviko 19 umetikisa sekta ya afya, rasilimali na maendeleo ya nchi yameelemewa na kuwa tafiti hizi zitawasaidia kugundua ukubwa wa tatizo, viashiria na athari za ugonjwa huu kwa jamii.
Kwa upande wa Familia ya Marehemu Amne Salim, Mtoto wake Ahmed Salim amesema mfuko huo umeunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na Uviko 19 kwa kuchangia kwenye tafiti zinazofanywa na Chuo cha MUHAS.
Salim amesema, mfuko huo utatoa kiasi cha Milion 100 kwa muda wa miezi 12 kuanzia Oktoba 2021 ili kusaidia tafiti za Uviko 19 na kutambua athari zinazosababishwa na ugonjwa huo.
Familia ya Dkt Salim Ahmed Salim imeamua kufanya kumbukumbu ya kifo cha Mpendwa wao Amne Salim aliyefariku Oktoba 20, 2020
Chuo cha MUHAS kimeweza kumkabidhi mtoto wa Amne Salim Tuzo ya ushirikiano wao na kutambua mchango kwa ajili ya mapambano ya Uviko 19 kupitia tafiti watakazozifanya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...