Kaimu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Apolinal Kamuhabwa akizungumza na watumishi wa Chuo hicho wakati wa mkutano uliolenga kutoa elimu ya Uviko 19  kwa watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam.






CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS)  kimetoa elimu ya Uviko kwa watumishi wa Chuo hicho na kusisitiza wapate chanjo ya Uviko 19 inayotolewa bure ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

MUHAS wametoa elimu hiyo kwa watumishi wa Chuo hicho kwa njia ya kufanya mkutano wa pamoja na wengine wakitumia njia ya mtandao na kutoa Chanjo ya Uviko 19

Akizungumza baada ya kumalizika, Kaimu Mkuu wa Chuo MUHAS Prof Apolonali Kamuhabwa amesema dhumuni kuu la kufanya mkutano huo na watumishi wa Chuo hicho ni kutoa elimu juu ya Uviko 19 na namna ya kujikinga.

Amesema mbali na hilo, Prof Kamuhabwa amesema wameshauri watanzania wapate chanjo ya Uviko 19 ili kupunguza uwezekano wa kulazwa na vifo.

Katika mkutano huo, Wataalamu mbalimbali wameweza kuzungumzia madhara yanayotokana na Uviko 19 ikiwemo shambulio la ini, moyo na hata Kisukari.

Mkutano huo uliweza kuendeshwa na Mtaalamu wa masuala ha Microbailojia na Immunolojia Prof Eligius Lyamuya ambaye amewahamasisha wanajumuiya na wanakamati wa MUHAS kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza maambukizi ya Virusi vya Uviko 19.

Prof Lyamuya amesema, watu wasikubali kupotoshwa kwani chanjo ya Uviko 19 ni nzuri na salama na imeweza kupunguza idadi kubwa ya Vifo.

Amesema, kwa watu waliochoma  chanjo ni wachache waliopata Maudhi madogo na kwa muda mfupi walirejea kwenye hali zao za kawaida.

Mbali na hilo, Prof Lyamuya amesema bado wanaendelea na tafiti mbalimbali ambapo kuna baadhi ya mataifa wameanza kutoa chanjo hizo kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 12.

Kwa upande wa utoaji wa Chanjo hiyo, Dkt Mariam amesema chanjo ya Uviko 19 haina madhara yoyote kwa wamama wajawazito wanapochoma ila anapopata maambukizi akiwa hana chanjo ya Uviko huwa anahatarisha maisha ya mama na mtoto.

Kufikia sasa Kuna chanjo 150, Chanjo 41 zikiwa katika majaribio na Chanjo 29 zikitumika kwa mataifa mbalimbali baada ya kupitishwa na Shirika la Afya duniani.

Kwa Tanzania ni asilimia 1 tu ya watanzania ambao wameshachoma chanjo hiyo huku wataalamu wakisisitiza elimu juu ya Maambukizi ya Uviko 19 yaendelee kutolewa kwa upana zaidi pamoja na madhara yake hususani kwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 50 na wenye magonjwa hatarishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...