
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) wamezindua wiki ya Huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Oktoba kila mwaka.
Akizungumza wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa, DKt. Elirehema Doriye amesema kuwa uwepo wa shirika la Bima la Taifa linategemea sana wateja kwa maana ya wadau mbalimbali wanaopata huduma kutoka shirika hilo.
"Sisi tunawahaidi kufanya maboresho zaidi ya huduma, mojawapo ya kauli mbiu yetu inayosema Mteja kwanza tutaweka katika kila shughuli zetu wateja na sehemu ya kwanza kabisa." Amesema Dkt. Doriye
Amesema wiki hii kwa pamoja na wateja washeherekee, wafurahie lakini kuwa alama ya kuonesha Shirika hilo linasimama kwaajili ya wateja wao, na kutoa elimu juu ya umhimu wa bima.
Hata hivyo Dkt. Doriye amewaasa jamii kujua shirika la bima la Taifa (NIC) kujua kuwa wao ndio Bima.
"Ni mhimu jamii na wateja wote wa bima kujua kuwa sisi ndio bima." Amesisitiza Dkt. Doriye
Licha ya hayo Dkt. Amewakaribisha wananchi wote kwaajili ya kupata huduma katika Shirika hilo la Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Yessaya Mwakifulefule amesema kuwa wanatambua mchango wa wateja wao.
"NIC tunaamini na kutambua kuwa wateja wetu ni zaidi ya wateja, ni washirikiana wetu. Wao ndio chanzo cha biashara na mafanikio ya nchini." Amesema Mwakifulefule
Amewasisitiza watumiaji wa shirika la Bima la Taifa Kuendelea kutumia Bima ya Taifa kwa maendeleo ya Taifa.
Mteja wa shirika la Bima la Taifa, Vedasto Rwegoshora amewapongeza shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kutambu kuwa NIC ndio Bima "Sisi ndio Bima" neno hilo linadhihirisha sasa kwani kumefanyika maboresho makubwa katika shirika hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha Keki Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akizungumza na wateja walioweza kufika katika Shirika hilo, katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akikata keki katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha keki mmoja wa wateja wa Shirika hilo, katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akilishwa keki na mmoja wa wateja wa Shirika hilo, katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mteja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Vedasto Rwegoshora akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha Keki Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akiwahudumia wateja wa Shirika hilo waliofika kwaajjili ya kupatiwa huduma katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha keki Mkurugenzi-Bima za Mali na Ajali (NIC) Bw.Ntimba Bunny katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi-Bima za Mali na Ajali (NIC) Bw.Ntimba Bunny akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.

















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...