Na Mwandishi wetu, Arusha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelea banda la Makumbusho ya Taifa katika Maonesho ya Utalii ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya TGT jijini Arusha.
Mhe. Dkt. Mwinyi akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Peter Mathuki.
Mhe. Mwinyi alionekana kufurahishwa sana na maelezo aliyopata kutoka kwa Mhifadhi Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Agness Gidna.
Wakati wote wa maelezo hayo alionesha kutikisa kichwa na kujibu kuwa sawa kabisa asante.
Dkt Gidna alimweleza Mhe. Dkt Mwinyi kuwa Makumbusho ya Taifa inafanyakazi ya kufanya utafiti, kukusanya, kuhifadhi na kutoa elimu kwa jamii kuhusu urithi wa asili na utamaduni wa nchi ya Tanzania.
“Karibu sana Mheshimiwa Rais, hapa ni Makumbusho ya Taifa na Idara ya Malikale, tupo hapa kwa ajili ya kutoa elimu ya urithi wa asili na utamaduni yaliyohifadhiwa na maeneo na malikale. Kwenye maonyesho haya tumekuja na vitu mbalimbali ikiwemo nakala ya fuvu la Zinjanthropus, zana za mawe za kale, marimba na mchezo wa bao kama mchezo wa asili wa Afrika..
Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro na yanafungwa leo na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt Hussein Mwinyi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...