KATIKA hali ya kushangaza! Wachezaji wa timu ya taifa ya Guinea Bissau wamejikuta kuugua matumbo huku wakiharisha na kutapika baada ya kula chakula cha jioni hapo jana wakiwa  kambini nchini Morocco kujiandaa na mchezo wao wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya timu hiyo.

Awali taarifa iliripotiwa kuwa idadi ya Wachezaji 25 wanaugua matumbo na baadae ilifahamika kuwa ni idadi ya Wachezaji Sita pekee waliokutwa na kadhia hiyo na tayari wapo Hispitali kwa matibabu zaidi.

Mchezo wao dhidi ya Morocco unatarajiwa kuchezwa leo majira ya Saa 4:00 Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki na Kati.

Timu hizo zipo Kundi moja, Kundi I na timu za Morocco, Guinea na Sudan. Huku Guinea Bissau wakiongoza Kundi wakiwa na alama nne, Morocco alama tatu, Guinea alama moja na Sudan hawana alama yoyote.

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...