KATIKA kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama na kutimiza malengo yao Taasisi ya Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAJIKI) limezindua mradi maalumu wa 'Safari Salama Bila Rushwa ya ngono' kwa wanafunzi na wanawake, mradi uliowahusisha madereva wa bodaboda na daladala kupitia vikundi vyao chini ya udhamini wa Women FundTanzania katika kuuunga mkono juhudi za mwanamke katika kupinga vitendo vya ukatili wa ngono kwa wanawake na wanafunzi ambao wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Janeth Mawinza  amesema, rushwa ya ngono ni changamoto kubwa kwa wanawake na wanafunzi na imesababisha wengi wao kutofikia malengo yao na ni jukumu la jamii nzima kushiriki katika kukomesha vitendo hivyo.

''Wanawake na wanafunzi wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa sana na rushwa ya ngono hasa wanapotoka majumbani na kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo elimu na ajira ajira ambapo wanakutana na wenye mamlaka katikati na kuwataka kutoa rushwa ya ngono ili waweze kupata huduma wanayohitaji....Tumeona mfano wa mdau mmoja hapa kuhusu madereva bodaboda wanapomtamani mtu hutumia nyenzo waliyonayo kuwasafirisha kwa malengo ya kuwalaghai na kupata rushwa ya ngono, hali hii hutokea pia shuleni, majumbani ambapo watu wanaotakiwa kuwapa huduma ndio huwaomba rushwa ya ngono'' Amesema.

Amesema, hali hiyo imewaibua na kuiamsha jamii kuelewa juu ya suala hilo ambalo limekatiza ndoto za watu wengi na kampeni hiyo imewashirikisha wadau hao pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU,) na kushauri namna bora ya kuangalia namna sahihi ya kumlinda mtoto wa kike dhidi ya rushwa ya ngono kwa kudai sheria ya mtoto kwa ulinzi zaidi  pamoja na TAKUKURU kuibadilisha sheria yao kwa kumweka mtoto salama zaidi. 

Vilevile amesema  suala la mapambano dhidi ya rushwa ya ngono na ukombozi wa mwanamke linapaswa kufanywa kitaasisi na jukumu la kila mmoja na kila kundi liongelee suala hilo ili liweze kutokomezwa ili kuleta mapinduzi.

Mradi huo umehusisha makundi maalum ya madereva wa daladala kupitia umoja wao wa UWAMAWIKI (Umoja wa Madereva wa Wilaya ya Kinondoni) na vikundi vyao ikiwemo; Umoja wa Madereva  wa Daladala Makumbusho, Tegeta, na Bunju (UWAMATEBU,) Umoja wa Madereva wa Daladala Makumbusho- Posta (UWAMAPO,) Umoja wa Madereva wa Daladala Mbagala (UMDM,) pamoja na Umoja wa Madereva na Pikipiki na Bajaji Gongolamboto.
Afisa Maendelea wa Manispaa ya Kinondoni, Zena Nalita akizungumza kuhusu namna Serikali ilinavyoshirikiana na Taasisi mbalimbali kwenye utoaji wa elimu ya kumlinda mtoto wa kike wakati wa kufungua warsha ya kutoa elimu kwa jamii. Bi Zena alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza  akizungumza kuhusu namna taasisi hiyo ilivyojipanga na kujikita kwenye kupambania mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto zake anapokuwa shuleni wakati wa hafla ya kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kumlinda mtoto wa kike.
Baadhi ya wazazi, madereva wa bodaboda na daladala wakisikiliza mjadala kuhusu kupinga vitendo vya ukatili wa ngono kwa wanawake na wanafunzi ambao wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameshika mambango ya kupinga ukatili wa kijinsia hata kwa mtoto wa kike.
Baadhi ya wazazi, madereva wa bodaboda na daladala wakichangia mada kwenye mjadala kuhusu kupinga vitendo vya ukatili wa ngono kwa wanawake na wanafunzi ambao wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya wanafunzi wakichangia mada
Idara ya Afya halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Grace Mampe aliyemwakilisha Mganga mkuu wa Kinondoni akitoa elimu ya chanjo ya Virusi vya Korona (UVIKO-19) kwa wananchi ili kuwaepusha na madhara yatokanayo na Virusi hivyo ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
 Mwakilishi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kamami  Ndaba akitoa neno la shukrani kwa wadau mbalimbali waliofika kwenye kwenye mjadala wa kupinga vitendo vya ukatili wa ngono kwa wanawake na wanafunzi ambao wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa.
Picha za pamoja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...