Baadhi ya wanasheria na wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, wakifuatilia Hotuba ya Rais wa Mahakama ya Afrika na haki za binadamu, Imani Aboud wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo na uelewa juu ya uwepo wa mahakama ya Afrika na sheria zake katika kutetea haki za binadamu. Semina hiyo imefanyika leo Novemba 13, 2021 katika ukumbi w Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.




MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu (African court) imeendesha semina kwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School)ili kuwajengea uwezo na uelewa juu ya uwepo wa mahakama hiyo ya Afrika na sheria zake katika kutetea haki za binadamu.

Akifungua semina hiyo, leo Novemba 13, 2021 Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu, Imani Aboud amesema lengo kubwa la semina hiyo ni kufahamishana, kuelezana, kupeana elimu na kubadirishana uzoefu ili kuwapa wanafunzi hao hamasa ya kwenda kufanya kazi ya uwakili kwenye mahakama ya Afrika.

"Semina hii tumeamua kuifanya hapa baada ya kuzingatia kwamba hawa ni wanafunzi, wanasheria ambao baada ya kumaliza masomo yao watakuwa wanasheria kwenye ofisi mbali mbali za serikali, binafsi, Kimataifa na wengine kujitegemea".

Amesema, suala la haki za binadamu ni la msingi linalitambulika katika nchi zote hivyo kuwaelimisha wanafunzi hawa kutambua kwa nini mahakama hii ilianzishwa na Mataifa ya Afrika ambayo ni wanachama wa umoja wa Afrika, sababu za kuanzishwa kwake, inafanya nini sheria na taratibu gani zinatumika itawasaidia kuja kuwa mawakili wazuri wenye elimu na ufahamu wa mambo ya haki za binadamu.

" Hawa ni kikazi kipya tunawaelimisha ili wakikuwa wawe wanajua hilo na baadae waje kuwa mawakili wazuri wenye elimu na ufahamu wa mambo ya haki za binadamu".

" Kama mnavyofahamu, elimu uzoefu ufahamu ni vitu ambavyo vinajengwa, lazima watu wafundishwe na waeleze na ndio maana maafisa wa mahakama wanatoa mafunzo ili kuwaeleza namna mahakama hii inavyofanya kazi na tunaimani kabisa baada ya hapa wanafunzi hawa watakuwa na wanauelewa mpana wa mahakama ya Afrika. Amesema.

Aidha amesema, zoezi hilo halijaanza leo, lipo kwenye utaratibu ambapo mahakama hiyo imekuwa ikisafiri kwenye nchi mbalimbali wanachama wa umoja wa Afrika na kutoa mafunzo pale tu fursa inapopatikana, kuweza kijadiliana na kuelimishana .

wa upande wake, mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo ( Law Shool) Benhaji Masoud amesema semina hiyo ya ya kutoa muamko kwa wanafunzi juu ya kazi za mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu itawasaidia sana kwa sababu katika masomo yao wanayoyasoma chuoni hapo kwa vitendo moja wapo ni haki za binadamu na uwepo wa mahakama za Kimataifa za haki za binadamu.

Amesema ujio wa mahakama hiyo na majaji chuoni hi hapo unawapatia fursa ya moja kwa moja kukaa nao na kuwauliza maswali kadhaa kuhusiana na kile walichokwisha soma na kupata ufafanuzi huku pia wakipata fursa nyingine ya kuongea na majaji ambao ndio hutoa maamuzi ya kesi, fursa ambayo siyo kila mtu anapata na hili ni ngumu kwa sababu wanafunzi hawa wanachokisoma hapa siyo elimu ile ya nadharia hii ni ya vitendo.

"Hawa wanafunzi wanaandaliwa kwa ajili ya kuja kuwa mawakili katika mahakama zetu hapa nchini na hata mahakama za kimataifa kwa kuwawakilisha wateja wao, hivyo kupata fursa hii ni swala muhimu kwao katika kujipanga, wakishapata hili mtu anaweza kujikuta anabobea katika eneo zima la sheri. Nawashauri waitumie fursa hii vizuri na waone kwamba huu ni mwanzo tu na watakapofuzu hapa kutekeleza majukumu yao hayaishii hapa nchini tu bali hata mahakama za Kimataifa

Naye Antony Colyuas mwanafunzi kutoka Taasisi hiyo amesema semina hiyo ni kubwa sana kwao kwani wamepata sehemu ya kujifunza kwa vitendo vile ambavyo wamekuwa wakijifunza darasanai.

Amesema pia wameweza kuona uhalisia wa kile ambacho wamekuwa wakisikia kupata interaction nzuri kutoka kwa watu (majaji) ambao wanatumaini kuja kuwa kama wao

Ameongeza kuwa mbali na kujifunza vitu ambavyo mahakama inafanya pia wamepata fursa ya kuzungumza na majaji .

Aidha aiomba serikali yetu kuendelea kuipa ushirikiano hii mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu kwa sababu inafanya kazi kubwa inatetea haki za binadamu na kuhakikisha haki inapatikana .

Naye, Aisa Foya amesema semina hiyo inawasaidia kuongezea ujuzi siyo kwa mahakama ya Tanzania pele yake kwani Mamahaka hiyo ya Afrika inajumuisha nchi tofauti tofauti na hivyo kuwapatia ujuzi na namna ya kwenda kupigania haki za watu mbali mbali wanaohitaji msaada wa kisheri kwa upande wa haki za binadamu.

"Mategemeo yetu makubwa kutoka kwenye semina hii ji kuongeza ujuzi ili kuja kusaidia watu wenye shida mbalimbali hususani kwenye masuala ya haki za binadamu na namna ya kujua sheria zake na kuifikia mahakama hiyo ili kuwapatia haki zao", amesema Foya.

Aidha amewashauri wenzake husani wale ambao bado wanasoma au wanatamani kusoma sheria kuendelea kujitoa na kuwa na utayari wa kuhudhuria katika semina ama debate ili kujifunza sheria katika upana wake.

"Leo hii tuko na majaji kutoka mahakama ya Afrika na haki za binadamu, kukutana na watu kama hawa inatupa upeo na nafasi kubwa zaidi ya kuweza kuhudhuri na kujua vitu vingine ambavyo tofauti na sheria inayotuongoza Tanzania peke yake". Amesema Foya.


Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za binadamu, Imani Aboud akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua semina kwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School) ili kuwajengea uwezo na uelewa juu ya uwepo wa mahakama ya Afrika na sheria zake katika kutetea haki za binadamu. Semina hiyo imefanyika leo, Novemba 13,2020 katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Aisa Foya, mwanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School) , akizungumza na waandishi wa habari namna semina ya kuwajengea uwezo na uelewa juu ya uwepo wa mahakama ya Afrika na sheria zake katika kutetea haki za binadamu itakavyowasaidia. Semina hiyo imefanyika leo, Novemba 13,2020 katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Anthony Colyuas, mwanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School) , akizungumza na waandishi wa habari namna semina ya kuwajengea uwezo na uelewa juu ya uwepo wa mahakama ya Afrika na sheria zake katika kutetea haki za binadamu itakavyowasaidia. Semina hiyo imefanyika leo, Novemba 13,2020 katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...