Na.Vero Ignatus,Arusha
Wataalam
wa wanayofanya kazi karibia ana mionzi wamepatiwa mafunzo maalum ili
kujikinga na madhara yanayotokana na athari za mionzi
Akizungumza mkuu wa Idara ya uhifadhi ya mabaki ya vyanzo vya mionzi mwishoni mwa Juma Jijini ArushaSalehe Mulisha ambae amemuwakilisha mkurugenzi mkuu wa TAEC aliwataka kutumia mafunzo hayo kujikinga na athari zitokanazo na mionzi
Amesema
lengo kubwa ni kuwakumbusha Usalama wa kazi katika maeneo yenye vyanzo
vya mionzi ,ambapo mafunzo hayo yanatoa Elimu ya kujikinga na Mionzi,
kwani kufanya kazi bila kuzingatia Usalama ,kunaweza kuleta madhara
makubwa kwa anaetumia sambamba na kwa wagonjwa wanaotumia
"Haya
ni mafunzo muhimu Sana kwasababu tulikuwa tunajaribu kuwakumbusha
wenzetu umuhimu wa kuzingatia masuala ya usalama wakati wa kufanya kazi
na vyanzo vya mionzi"Alisema Salehe
Nae Mratibu wa mafunzo hayo ambae pia ni mtafiti katika Tume ya Nguvu ya Atomic Wilbroad Mlogora (TAEC
) anamsema mafunzo hayo yanalenga kuinua uelewa wa Kinga ya mionzi kwa
wafanyakazi, ambao wanafanya kazi kwenye Tiba kwa njia ya X-Ray,kwani
wao nitofauti na wafanyakazi wengine,kwani wao na mgonjwa wanakuwa
chumba kimoja, hivyo upo uwezekano mkubwa Kama wasipopata mafunzo ya
namna ya kujikinga wakapata madhara.
Kwa kuzingatia hayo madhara yanaweza kuepukika ,Ila kupata mionzi hakuwezi
kuepukika ,kwani inafahamika kila kitu kina madhara na faida zake,hivyo
wanao uhakika kutokana na mafunzo hiyo mionzi kidogo wanayoipata,
haitaweza kuwaletea madhara .
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo Idrisa Juma kutoka
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,ambae ni Afisa mteknolojia wa Elimu
ya mionzi , alisema kuwa kutokana na Elimu waliyopatiwa imezidi
kuwaongezea weledi na ufanisi katika ufanyaji wa kazi, kwasababu huwa
wanaendesha mitambo ya mionzi katika tiba na katika upimaji,hivyo
itawasaidia kuwakinga wengine dhidi ya mionzi
Martha Emmanuel Mbona yeye ni
muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,anasema yeye anafanya
kazi katika chumba ambacho wanatumia mionzi na wanashughulika na
utambuzi, uchunguzi wa mishipa ya damu ya Moyo pamoja nakuziba matundu
madogo ya Moyo haswa kwa watoto na watu wazima
Hivyo
Mafunzo hayo yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi kwani yeye ni mtu
wa pili kutoka kwa Daktari ,hivyo itamsaidia kujilinda na mionzi
kwasababu wanapoendelea na kazi katika chumba wanakuwa pamoja na
mgonjwa, hivyo Ile mionzi anayoioata mgonjwa anategemea itanipata japo
kwa kiasi kidogo,kwani mafunzo aliyoyapata yatamsaidia jinsi gani
itapungiza Ile dozi iwe kwenye dozi ndogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...