Na Khadija Kalili, Kibaha
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani RPC Wankyo Nyigesa ametoa amri kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani kwa Kila anayemiliki silaha kinyume cha sheria aisalimishe silaha yake kwa hiari katika vituo vilivyo karibu ikiwa ni pamoja na Ofisi za serikali za mtaa, Ofisi za serikali za vijiji na Ofisi za Kata.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari leo alisema kuwa zoezi hilo lilianza Novemba mosi mwaka huu na litafikia tamati Novemba 30 na baada ya tarehe hiyo msako mkali utafanyika na atakaekaebainika anamiliki silaha kinyume cha sheria hatua kali zitachukuliwa.
RPC Wankyo alisema kuwa wamebaini kuwa kuna baadhi ya Kampuni za ulinzi binafsi zinazotumia silaha zisizoruhusiwa kutumia silaha zisizoruhusiwa kutumia katika ulinzi huku alizitaja baadhi ya silaha hizo kuwa ni gobole, rifle na short gun.
"Tunatoa rai wamiliki wa Kampuni hizo wazihusishe na kusajiri silaha zinazopendekezwa ambazo ni shortgun pump action na Kampuni itakayoshindwa kuhuisha silaha zake itafutiwa usajili wa kumiliki Kampuni hizo"alisema RPC Wankyo.
Wakati huohuo RPC alisema kuwa wamefanya msako katika Wilaya Tano za Polisi Ili kudhibiti na kuzuia matukio mbalimbali ambapo pia wamekamata not bandia 108 (dola 100 Kila), simu 7 za aina mbalimbali, nyara za serikali meno ya tembo2, bangi Puli 13, kete 272 na kilo 172, gongo Lita 93.5, mifuko 20 ya saruji, Ndoo 6 za rangi ya maji, TV mbili aina ya A order, Kompyuta mpakato 1aina ya Toshiba.Pia amewataka wananchi wote wanaomiliki vyombo vya moto kupeleka kwenye ukaguzi katika vituo vya Polisi Ili vikaguliwe ukaguzi huo inafanyika bure na baada ya ukaguzi muhusika atalupia stika ya usalama barabarani na kulipia sh.3000 gari ndogo na 5000 gari kubwa,wiki ya nenda kwa Novemba 21 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...