Na Khadija Seif, Michuzi Tv
WASANII wanaoingia ubia na Kampuni na Mataasisi mbalimbali nje na ndani ya nchi hususani bidhaa kwa matumizi ya binadamu watakiwa kutumia bidhaa hizo kabla ya kukubali kazi ya kufanya ushawishi na hamasa kwa watumiaji ili kujenga uhakika na matumizi salama.
Akizungumza na Michuzi Tv Zamaradi Mketema ambae rasmi ametangazwa kuwa Balozi wa Kampuni ya "Astra" inayojihusisha na bidhaa za Usafi kwa kutengeneza Sabuni kwa Mahitaji mbalimbali amesema haikuwa rahisi kwake kuweka maslahi mbele kuliko kupotosha jamii kutoka na Kampuni inayoingia nae ubia katika kutangaza bidhaa zao kutokana na Imani aliyoijenga kwenye jamii inayozungumza.
"Ilinichukua muda Sana kukubali kuwa Balozi ilinibidi nijaribu kwanza kutumia bidhaa zao ikiwemo Sabuni ya kusafisha Sakafuni,ya kuoshea vyombo,vitakasa vya mikono pamoja na Sabuni ya kunawa mikono na kuona ubora wake ambapo Haina madhara kwa mtumiaji".
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya"Astra" Shamsa Akukweti ameeleza kwa namna gani wameweza kumpatia nafasi Zamaradi ya ubalozi wa bidhaa zao huku akifafanua zaidi kwa jinsi walivyokua wakifatilia Mienendo na ushawishi wa Mwanadada huyo katika jamii
"Ni mwanamke,ni mama anayejituma, Mchapakazi na Cha mwisho ni msafi kama anavyoonekana katika maisha yake pia ni mtu mwenye ushawishi."
Pia amefafanua Mkataba huo baina ya Zamaradi na Kampuni yao ni wa kipindi Cha miezi 6 ambapo atatangaza bidhaa zao kupitia mitandao yake ya kijamii pamoja na kugawa zawadi kwa watu maarufu ikiwemo ni sehemu ya kuzitangaza bidhaa za Sabuni ikiwemo Sabuni ya Mikono,vyombo pamoja na zingine nyingi.
Mkurugenzi wa Kampuni "Astra" inayojihusisha na kutengeneza bidhaa za Usafi ikiwemo Sabuni Ahmad Atallah akiwa pamoja na Balozi wa Kampuni hiyo Zamaradi Mkema wakinyanyua Mikataba yao ikiwa ishara ya kufanikisha kukubali kufanya kazi pamoja ya kutangaza bidhaa hizo.
Zamaradi Mketema akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Balozi wa Kampuni ya "Astra" inayojihusisha na kutengeneza bidhaa za Usafi ikiwemo Sabuni kwa Matumizi mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...