Na Mwandishi wetu.

Mkuu was Wilaya ya Ubungo Kheri James Amesema kuwa Amani iliyopo Tanzania inatokana na uwepo wa dini na maombezi mbalimbali ya kuliombea Taifa letu.

DC James Amesema hayo Leo jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa kanisa la ngome ya Yesu kristo lililopo Kimara Temboni Kwa Richard Mwacha.

DC James Amesema kuwa katika Ibada hii anampongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa uongozi wake Kwa kutimiza miezi 9 Ikulu akiboresha mambo mbalimbali ikiwemo Uchumi, Demkrasia , Uhuru wa kujieleza na Haki za binadamu.

"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaamini kuwa dini kuwa ni mkombozi na msingi mkubwa wa Amani na utulivu uliopo nchini Tanzania.

Amesema kuwa anawatoa wasiwasi kuwa serikali itaendelea Kushirikiana na dini zote na Rais anaamini kuwa dini zina mchango mkubwa wa kulifanya Taifa kuendelea kuwa na amani.

"Aidha niombe kuwasihi watanzania kamwe wasikubali kudanganywa na watu wasio litakia mema Taifa letu Kwa ujumla" Amesema DC James.

Kwa upande wake kiongozi wa kanisa Hilo Kuhani Richard Mwacha Amesema kanisa lake Lina maono ya kujenga jengo la ghorofa tatu litakalo chukua watu 15,0000.

Ametaja kuwa gharama halisi ya ujenzi wa jengo Hilo ni Billion 5 za kitanzania.

Ameishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Mama Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa uhuru wa kuabudu.

Pia ameishukuru serikali kupitia kiongozi wake wa Wilaya ya Ubungo Kheri James Kwa kuendelea kuwa na ushirikiano Kwa tasisi za dini na kanisa Hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa ujenzi wa kanisa la Ngome ya Yesu.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akizungumza na waumini wa kanisa la Ngome ya Yesu Kristo Kimara Temboni




Waumini wa kanisa la Ngome ya Yesu kristo lililopo Kimara Temboni Wakiwa katika Ibada ya kristmas
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akiwa ameongozana na Viongozi wa kanisa la Ngome ya Yesu kristo lililopo Kimara Temboni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...