Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

BONDIA kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Selemani Kidunda amesema namna bondia anavyokuja ndivyo atakavyompokea.

Ameyasema wakati wa kupima uzito wa pambalo la la mkanda wa WBF International dhidi ya Bondia kutoka Demokrasia ya Congo Eric Tshimanga Katompa litakalofanyika Kesho Jijini Dar es Salaam.

Kidunda amesema katika pambano lake amejiandaa vya kutosha na amehaidi kutokuwaangusha watanzania.

Pambano la kupigania mkanda wa WBF International, raundi 10 uzito wa kilo 76 kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza.

Akizungumza baada ya kupima uzito leo bondia huyo ambaye amesema kuwa anatarajia kushuka ulingoni akiwa tayari na maandalizi ya kutosha kwani yeye ametumwa kazi na atafanya kazi.

Kwa upande wa Bondia kutoka Congo Tshimanga Katompa amesema kuwa  atahakiksha anafanya vyema kesho katika pambano hilo.

Kwani lengo kuwa ni kihakikisha anaibuka na ushindi wa pambano hilo.

Huku kwa upande wa mabondia wengine katika uzito wa kg 62 Leila Yazidu dhidi ya Najma Isike, Pascal Manyota vs Joseph, Idd Jumanne alipima uzito huku mpinzani wake Hamisi Kibodi hakuweza kutokea.

Israel Kamwamba ameshindwa kuja sababu ya hali ya sasa kuvuka mipaka yetu, kushinda kupata ruhusa nchini na mabadiliko Bondia Ibrahim Class atapambana na Kelvin Majiba uzito wa 66. pambano lingine ni Ruth Chisale wa Malawi dhidi ya Grace Mwakamele uzito wa Kg 63 raundi 8 ubingwa wa wanawake PST huku Juma Choki 62 dhidi ya Saluma Chazamba wa Malawi.

Pambano lingine ni Paul Magesta vs Oscar Pascal raundi 8,Hassan Milianzi vs George bonabucha wakiwania ubingwa wa PST ubingwa, Ismail Gariatano vs Denis Mwale ubingwa wa PST.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...