Na.Khadija Seif, Michuzi TV
SHINDANO la Kumsaka Mrembo atakaewakilisha Afrika Mashariki (Miss East Africa) linatarajiwa kufanyika mkesha wa Christmas disemba 24 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kilimanjaro Jijini Dar es salaam Muandaaji wa Shindano hilo ambae pia alishawahi kuwa Miss Rwanda mwaka 2016 Jolie Mutesi amesema Kwa mwaka huu imejumuisha Warembo kutoka Mataifa 16 ikiwemo Kenya,Uganda,Burundi,Sudani kusini, Tanzania, Ethiopia,Somalia,Djibout,Visiwa vya Comoro,Sea shells,Eritrea,Malawi
Mutesi akafafanua zaidi mchango wake katika tasnia ya Urembo ni kuona Kwa jinsi gani Urembo unaweza kuchukua nafasi kubwa katika kubadilisha Mila potofu katika jamii ikiwemo swala la ukeketaji,ukandamizaji,ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.
"Warembo wote watapewa nafasi ya kuonyesha tamaduni za nchi yao,ikiambatana na kujibu maswali ya papo Kwa hapo wakiwa jukwaani japo Kila Mshiriki anakua na program yake ya kusaidia jamii wengine wanajikita kwenye Elimu,Afya ya watoto na wakina Mama hivyo Warembo wataweza kupewa nafasi kutambulisha program zao katika jamii."
Hata hivyo Mutesi ameeleza Kwa namna ya upatikanaji wa Warembo hao ilijikita zaidi kwenye Mrembo ambae anaweza kuzungumza lugha zaidi ya mbili hususani kuzingatia lugha ya Kiswahili.
Pia ameongeza kuwa Atakaeibuka Mshindi atajizawadia gari mpya aina ya "Nissan X trail mpya Huku walioshiriki kupata kifuta jasho Kwa kila mwezi ikiwa ni sehemu ya kumthamini ushiriki wao na usiku huo utapambwa Kwa burudani nyingi ikisindikizwa na Msanii Fere gora kutoka demokrasia ya Kongo pamoja na Mbosso kutoka nchini Tanzania.
Aidha,Mratibu wa Shindano hilo Kwa upande wa Tanzania Hellen Kazimoto amefafanua zaidi viingilio Kwa wadau na wapenzi wa tasnia ya Urembo Ili waweze kujitokeza Kwa wingi katika usiku huo wenye Warembo wawakilishi kutoka nchi mbalimbali na ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nchi Tanzania.
"Kiingilio kuanzia shilingi elfu 50 Kwa mtu Mmoja na,laki 2 Kwa meza na tiketi zinapatikana vituo kama Wasafi, Vunjabei pamoja na Mtandaoni.
Muandaaji wa Shindano la Taji la Mrembo wa Afrika Mashariki (Miss East Africa) Jolie Mutesi akizungumza na waandishi Wahabari na kueleza namna Msanii kutoka Jamhuri ya demokrasia ya Kongo Ferre gora pamoja na Mbosso kutoka nchini Tanzania watakavosindikiza usiku huo wa fainali ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mkesha wa Christmas disemba 24 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa Shindano la Taji la Mrembo wa Afrika Mashariki (Miss East Africa) Muandaaji wa Shindano hilo Jolie Mutesi pamoja waratibu wa Shindano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...