Kuna mjadala unaoendelea kuhusu nchi kukopa au kutokukopa. Kama mwananchi wa kawaida nani ningependa kutoa mtazamo wangu kwa faida ya wote.
Kwanza ni muhumu ikafahamika kwamba HAKUNA nchi duniani inayotekeleza miradi ya maendeleo bila kukopa. Hata nchi tajiri ulimwenguni zinakopa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Takwimu za Mkopo wa dunia (global debt) za mwaka 2020 zinaonesha kwamba nchi tajiri ndio zilizoongoza kwa kukopa.
Marekani peke yake deni lake lilikuwa asilimia 31.8 ya deni la dunia; Japan deni lao lilikuwa asilimia 18.8 ya deni la Dunia; Uingereza share yao ilikuwa ni asilimia 3.7; Ufaransa ailikuwa asilimia 3.8. Nchi 54 za Afrika deni lao kwa pamoja (combined) ni asilimia 2 tu.
Hiyo ndio sababu hadi leo Afrika tunakabiliwa na changamoto za kutokuwa na barabara za kutosha, hatuna reli za kutosha; hatuna maji ya kutosha; hatuna vituo vya afya vya kutosha; hatuna madarasa ya kutosha nk
Wakati nchi za Afrika hazikopi vya kutosha ili kuweka hiyo miundombinu ya msingi; nchi tajiri zilizoendelea wanakopa ku-upgrade miundombinu ambayo tayari wanayo.
Kwa mfano hivi sasa China wanayo reli ambayo treni inasafiri kwa spidi ya km 300 kwa saa; sasa wamekopa kujenga reli yenye spidi ya kilomita 600 kwa saa. Sasa kuna kosa gani sisi kukopa kujenga barabara?
Kama Nchi tajiri zinakopa kuvumbua teknolojia itakayofanya uzalishaji viwandani ufanywe na robot badala ya binadamu- kuna kosa gani sisi kukopa kwa ajili kujenga madarasa yatakayosaidia watoto wetu wasome kwa staha? Kama wenzetu wanakopa kwa ajili ya kwenda Mwezini; kuna ubaya gani sisi kukopa kujenga reli ya Kaliua-Mpanda-Kalema? Kuna ubaya gani kukopa kupeleka Maji Tabora; Dodoma; Singida; Rukwa nk. Binafsi sioni ubaya.
Hivyo ni muhimu sana kuielewa dhana ya nchi kukopa sio jambo geni na wala sio jambo baya na kila nchi duniani inakopa.
Mdau Mbelwa Kairuki
Mbelwa Kairuki
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...