Na. John Mapepele
Mikoa yote ya Tanzania
Zanzibar na zaidi ya mikoa kumi Tanzania Bara inashiriki michezo ya sanaa za
maonesho inayoanza kesho kwenye mashindano ya Taifa CUP 2021 inayoendelea jijini
Dara es Salaam hivyo kuleta vionjo vya aina yake katika mashindano ya mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo, Omary Yusufu Singo ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Michezo nchini kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari leo, Disemba 13, 2021
kwenye ukumbi wa mkutano wa Uwanja wa Benjemini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Singo amesema mashindano ya mwaka huu ambayo yameshirikisha michezo ya Soka kwa wanaume na wanawake, netiboli na riadha yameongezewa vionjo kwa kushirikisha sanaa za maonesho ambazo zitashindanisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ili kuibua vipaji katika fani za muziki wa Singeli na Muziki wa kizazi kipya.
Mratibu waTamasha hilo la
Sanaa za maonesho, Bi Leah Kihimbi ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Maendeleo ya Sanaa nchini amesema kuwa mashindano hayo siyo tu yanaongeza radha
mpya ya Taifa CUP 2021 bali yatasaidia kutoa fursa ya pekee kwa wasanii ambao
watatumbuiza na kubahatika kupata nafasi za kuendelezwa.
Amesema mashindano hayo yanatarajia
kuwa ya siku mbili na kuanza kesho na yatakuwa yakifanyika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
kuanzia saa moja usiku.
Ametoa wito kwa vyama na
mashirikisho mbalimbali kutumia nafasi hii kuja kupata vipaji ambavyo wanaweza
kuviendeleza ili kufanya vizuri zaidi kwenye ngazi za kimataifa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya
Ufundi ya Taifa CUP 2021 Jackson Ndaweka ambaye pia ni Katibu wa Shirikisho la
Riadha Tanzania amesema kwa upande mchezo wa soka wanaume tayari
timu za Mara na Mjini Magharibi zimefuzu
kuingia nusu fainali leo wakati soka wanawake timu ya Mkoa wa Dar es
Salaam imekuwa timu ya kwanza kufuzu kuingia nusu fainali baada ya kuichabanga
Mjini Magharibi magoli 2-1.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa CUP 2021 Yusufu Omary Singo (katikati) wakiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya Taifa CUP Jackson Beda (kushoto) na Leah Kihimbi (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa Sanaa kwenye mkutano na waandishio wa habari kuzungumzia Uzinduzi wa Sanaa za maonesho kwenye Taifa CUP hapo kesho jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...