Mkuu wa Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda akimtunuku Shahada ya Uzamili Daktari Bingwa wa Watoto Kamlesh Kara wakati wa mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya chuo hicho. Kushoto ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Charles Mgone.
Wahitimu wa fani mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) wakila kiapo cha uaminifu katika fani yao wakati wa mahafali ya 19 yaliyofanyika chuoni hapo Mikocheni Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), wakisimama kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mahafali ya 17 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya chuo hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam . Wa kwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Charles Mgone, Mkuu wa chuo Anne Makinda, Mwenyekiti wa Mtandao wa Eli ya Afya Kairuki (KHEN), Kokushubira Kairuki na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, John Ulanga.
Wahitimu wa fani mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) wakila kiapo cha uaminifu katika fani yao wakati wa mahafali ya 19 yaliyofanyika chuoni hapo Mikocheni Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), wakisimama kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mahafali ya 17 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya chuo hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam . Wa kwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Charles Mgone, Mkuu wa chuo Anne Makinda, Mwenyekiti wa Mtandao wa Eli ya Afya Kairuki (KHEN), Kokushubira Kairuki na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, John Ulanga.
Wahitimu wa fani mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), wakiingia kwa maandamano kwenye mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KAMA hatua ya kuendelea kujiimarisha Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimefadhili masomo ya wahadhiri wake 13 ndani na nje ya nchi kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu (PhD).
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Charles Mgone wakati wa mahafali ya 19 yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Jumla ya wahitimu 309 walitunukiwa Vyeti, Stashahada, Shahada, Shahada za Uzamili baada ya kufuzu taaluma zao kwa mwaka wa masomo wa 2020/2021.
Wahitimu 84 walitunukiwa Stashahada ya Uuguzi, 43 Shahada ya Uuguzi, wahitimu 171 walitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Binadamu, 7 Shahada ya Uzamili ya Udaktari wa Binadamu katika Tiba na Afya ya Watoto, 3 Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Afya ya Jamii na mmoja Shahada ya Uzamili ya Ustawi wa Jamii.
Amesema wameamua kusomesha wahadhiri wake ili kuimarisha shughuli za ufundishaji, utafiti na utoaji wa ushauri kwa Jamii na kwamba ili kuen delea kujiweka kwenye nafasi nzuri HKMU itaendeleza juhudi zetu za kuwasomesha wafanyakazi.
Ameongeza kuwa, kwa upande wa shughuli za utafiti, Chuo kimeendelea kufanya tafiti mbalimbali kupitia kwa wanataaluma pamoja na wanafunzi wa ngazi zote na kwamba mwaka huu wataalam wake wametoa machapisho mbalimbali licha ya majukumu mengine waliyo nayo ya kufundisha wanafunzi na kutoa ushauri.
“ Tutaendelea kuliwekea mkazo eneo hili kwani ni jukumu mojawapo la msingi wa kuwepo kwa Chuo Kikuu. Kwa niaba ya Chuo napenda kuwapongeza wanataaluma na wanafunzi wote kwa machapisho hayo ambayo yametambulika kitaifa na kimataifa na kukiletea chuo na Taifa kwa ujumla sifa kubwa,” amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la HKMU, John Ulanga yeye amemshukuru Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Charles Mgone kwa utumishi uliotukuka wa kukiendesha chuo hicho kwa umahiri mkubwa.
“Nakumbuka ilivyokuwa ngumu kukuomba ujiunge nasi miaka mitano iliyopita maana ulisema umeshamaliza majukumu yako kimataifa na sasa umerudi nyumbani kupumzika lakini baada ya kukubembeleza ukakubali kuwa nasi kwa hii miaka mitano nakupongeza sana,” amesema
Ulanga amesema kwa miaka aliyokaa chuoni hapo amekiwezesha chuo hicho kuboresha taaluma na vifaa vya kufundishia na kusaidia kupatikana kwa wahadhiri wengine wa fani mbalimbali.
Mwenyekiti huyo pia ameishukuru Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu HESLB kwa kuendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wa chuo hicho na wa vyuo vingine na kwamba mikopo hiyo isingekuwepo basi idadi ya wahitimu wa chuo hicho ingekuwa ndogo.
“Hata hivyo nitoe rai kwa serikali kutupia jicho sekta ya elimu kwa wataalamu wa afya kwa kutoa mikopo na ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchinikwa idadi kubwa zaidi. Ni kweli kabisa kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma kwenye chuo chetu kwa mwaka huu walipata kiasikidogo sana cha mkopo hasa kwenye ada,” alisema Ulanga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...