Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti ametoa ushauri huo (22.12.2021) mjini
Sumbawanga wakati akizungumza kwenye kikao cha kusimamia, kuratibu na kudhibiti
mapato na matumizi ya serikali robo ya pili kilichohudhuriwa na wakurugenzi wa
halmashauri zote.
“Mvua
zimechelewa sana. Katika wilaya zetu tumeshuhudia kiwango kidogo cha mvua hadi
sasa hivyo ni wakati muafaka wataalam wa kilimo wakaelimisha wakulima kupanda
mazao yanayostahimili ukame “alisisitiza Mkirikiti.
Mkirikiti
aliongeza kusema tayari serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo kugawa mbegu za
soya na alizeti ili wakulima wazalishe mazao hayo ambayo haihitaji mvua nyingi
na kuwa jitihada zaidi zinatakiwa ikiwemo kutumia kilimo cha umwagiliaji katika
mabonde yaliyopo ili kuwa na uhakika wa mazao ya chakula.
Katika
hatua nyingine Mkirikiti amewagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo
kukamilisha miradi ya ujenzi wa madarasa chini ya mpango wa Maendeleo ya Ustawi
wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 ili yatumike kupokea wanafunzi wa
kidato cha kwanza mwaka 2022.
Kuhusu
kuongeza mapato ya halmashauri, Mkirikiti amewataka wakurugenzi hao kujikita
katika kubuni vyanzo vipya visivyo kuwa kero kwa wananchi ili miradi ya
maendeleo itekelezeke.
Kwa
upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Denis Bandisa akizungumza kwenye kikao
hicho aliwakumbusha viongozi wa halmashauri kuendelea kutenga fedha na
kutekeleza afua za lishe ili kuondokana na tatizo la udumavu na utapiamlo kwa
watoto chini ya miaka mitano.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...