Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.
Uongozi
wa serikali ya Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
umesema umeendelea kushirikiana na serikali na mamlaka zake katika
jitihada za kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia .
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Mtaa huo Solomon Najulwa ambaye amesema
viongozi na wakazi wa mtaa huo wamekuwa mstari wa mbele katika mapambano
dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Amesema kutokana
na elimu sahihi waliyopatiwa wakazi wa mtaa huo kuhusu madhara ya
ukatili jamii imekuwa na uelewa mkubwa kuhusu namna ya kukabiliana na
matukio ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa pale inapojitokeza
mtu kuhusika au kufanyiwa ukatili.
“Kama kunaukatili wowote
ndani ya ngazi ya familia iwe baba anafanyiwa ukatili na mke wake avunje
ukimya lakini pia kama kunawatoto ambao wapo katika ngazi ya familia
ambao wanaishi maisha magumu wametelekezwa na wazazi wao na wanashindwa
sehemu ya kusemea waje kwenye ofisi yangu ya serikali ya mtaa lakini pia
hata kama kunajirani ameona jirani yake anafanyiwa ukatili naomba
tafadhari avunje ukimya”.
“Ukatili wa kijinsia na unyanyasaji na
mambo mengine mengi ambayo niya jinai sisi tunayatoa na kuyapeleka
sehemu husika tunafanyakazi vizuri na jeshi letu la polisi tunafanyakazi
kwa ushirikiano mzuri pamoja na vitengo vyote dawati la jinsia na
watoto pamoja na ustawi wa jamii”.
Hata hivyo mwenyekiti huyo
amesema pamoja na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kama
hatua ya kudhibiti ukatili lakini bado kuna viashiria vya unyanyasaji wa
kijinsia ikiwemo mifarakano ya wanandoa ambayo imekuwa ikiathiri
familia.
“Mtaa wangu umepiga hatua ya mafanikio ila bado
kunaviashiria vingi kwenye familia kama vile kuna baadhi ya wazazi
wanapotalakiana huziacha familia zao hasa wale watoto wasijue la kufanya
na pia watoto kutawanyika hovyo na kuanza kulanda landa mtaani pamoja
na kujihusisha na mambo ambayo hayana maadili”.
Serikali na wadau
mbalimbali wa kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia wameendelea na
maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia
ambao kilele chake Disemba 10 mwaka huu.
Home
JAMII
SERIKALI YA MTAA DOME SHINYANGA WAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPINGA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...