Mwandishi wetu, Arusha
WAANDISHI wa habari na watangazaji juzi wamepata chanjo ya ugonjwa wa uviko-19 ,huku wakitakiwa kujali afya zao kwanza katika utendaji kazi kwani afya ndio mtaji wao.
Chanjo kwa wanahabari, imetolewa na madakari hospitali ya wilaya Arumeru na Jiji la Arusha baada ya kutoa semina juu ya umuhimu wa chanjo huku wakiwataka wanahabari kusaidia kuelimisha umuhimu wa chanjo nchini.
Zoezi hilo la chanjo ilikuwa ni sehemu ya mafunzo kwa wanahabari yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la utetezi wa haki za Binaadamu la DefendDefenders kwa kushirikiana na Taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii ya pembezoni (MAIPAC) ya Mkoani Arusha.
Dk Pascal Kang'iria alisema wanahabari wanajukumu la kuelimisha juu ya umuhimu wa chanjo ili kuondoa upotoshwaji katika jamii.
"Nimefurahi sana Leo kukaa na nyie wanahabari kwani nyie mkijua umuhimu wa chanjo mtatusaidia sana kuelimisha jamii huko mtaani Kuna habari nyingi za kumpotosha"alisema
Afisa Kitengo ya Ulinzi na Ustawi wa shirika la DefendDefenders East and Horn of Africa, Karis Moses alisema wanahabari wanaopaswa kuthamini afya zao kwanza ni kwani ndio mtaji wao.
Moses alisema kazi za Uandishi wa habari na utangazaji zinakawaida kuwa changamoto ambazo husababisha msongo wa mawazo na hata kupata Maradhi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC)Mussa Juma Shirika hilo limejipanga kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa chanjo wa wanahabari , mashirika yasiyo ya kiserikali (CSOs) na jamii kwa ujumla.
Juma alisema wanahabari wakijua wajibu wao katika jamii watasaidia kupunguza changamoto ikiwepo upotoshwaji juu ya ugonjwa wa uviko-19 na Chanjo na hivyo Wananchi wengi kujitokeza kupata chanjo.
Alisema katika jamii za wafugaji wa asili na wawindaji bado hakuna elimu ya kutosha ya Chanjo hivyo MAIPAC kwa kushirikiana na radio za kijamii katika maeneo hayo na viongozi wa Mila imejipanga kutoa elimu ili kudhibiti kusambaa ugonjwa wa uviko-19.
Waandishi wa habari 20 kutoka mikoa Saba wanashiriki mafunzo sehemu ya Mradi kuwajengea Uwezo watetezi wa haki za Binaadamu nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...