………………………………………………………………
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Wanafunzi 3,404 waliofaulu darasa la saba katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wanategemea kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja kutokana na ujenzi wa madarasa 47 yanayojengwa katika Halmashauri hiyo.
Akiwa ziarani Wilayani humo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amekagua ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa katika shule ya Sekondari Gumangwa kwa niaba ya vyumba vyote 47 vilivyojengwa katika Halmashauari hiyo.
Kutoka katika mradi wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imepoeka shilingi Milioni 940 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 47 katika shule za Sekondari Wilayani humo.
Akiwa shuleni hapo Waziri Ummy ameridhishwa na ujenzi wa madarasa hayo na amepongeza Uongozi wa Manispaa ya Singida kwa usimamizi makini wa ujenzi wa madarasa hayo.
Naye Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Gumangwa Mwl. Lucas Egugu amesema wanafunzi waliomaliza kidato cha nne katika shule hiyo ni 77 na waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza ni 245 lakini kwa ujenzi wa madarasa hayo 7 yatapawezesha wanafunzi wote kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja.
Pia amemshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha walizopata kwa kuwa zimeongeza fursa za Elimu kwa watoto wote wa Kitanzania kupata elimu yao kwa wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...