Na Jane Edward,Arusha.

Wananchi na mkoa wa Arusha na mikoa jirani wametakiwa kutumia fursa  katika msimu huu wa sikukuu ya kununua bidhaa zilizo bora na zenye viwango vikubwa ambazo ni rafiki kwa mazingira .

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi mtendaji kampuni ya vifaa vya LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim wakati akizungumza katika  hafla ya uzinduzi wa duka jipya la vifaa vya LG kwa kushirikiana na  Kampuni ya Benson lengo likiwa ni kuwasogezea huduma  karibu  wateja wao vikiwa na viwango na ubora wa hali ya juu.

Kim alisema kuwa,kwa zaidi ya  miaka 41 Sasa kampuni ya Benson wamekuwa wauzaji wakuu wa bidhaa  za kampuni ya LG mkoani Arusha lengo likiwa ni kuwasogezea huduma kwa karibu  wateja wake.

Kim alisema kuwa,hiyo ni mara ya kwanza  kwa kampuni hiyo ya LG kuzindua duka hilo mkoani Arusha baada ya kuzindua maduka mengine matatu jijini Dar es Saalamu mwaka huu lengo likiwa ni kusambaa Tanzania nzima.

"Bidhaa hizi tulizozindua hapa leo ni TV za kisasa,friji ,mashine za kufulia nguo ambapo vifaa hivyo vimetengenezwa kisasa zaidi na  zinatumia umeme mdogo sana na tunaahidi wateja wetu kuwa miezi michache ijayo tuna mpango wa kufungua maduka mengine ya LG katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuwapatia huduma wateja wetu"alisema Kim.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa bidhaa za umeme ya Benson Ltd ,Nadeem Hussein alisema kuwa,wamekuwa wakitoa huduma zilizobora  na za uhakika kwa wateja wao katika kuuza bidhaa zinazomgusa kila mtu .

Nadeem amempongeza Rais Samia kwa namna ambavyo amefungua fursa za kufanya biashara katika nchi mbalimbali na hivyo kupanua wigo wa wafanyabiashara kufanya biashara kwa Uhuru bila kusumbuliwa na mtu yeyote.

"bidhaa zetu tunazouza zina ubora wa hali ya juu na zinapunguza matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa Sana ,na pia gharama zetu zinamfanya mteja yotote kuweza kununua , hivyo tunawaomba wateja wajitokeze kwa wingi kuja kununua ."alisema Nadeem.

Meneja wa duka la LG Benson Arusha,Zahra Mohamed alisema kuwa,bidhaa hizo zina manufaa makubwa sana kwani ni rafiki kwa mazingira na ni za kisasa na wametoa punguzo la bei kwa asilimia 20 kwa bidhaa zao zote katika msimu huu wa sikukuu ili wateja waweze kupata huduma hizo kwa urahisi zaidi.

Mkurugenzi mtendaji Benson LTD Akizungumza kuhusiana na ujio wa duka jipya la bidhaa za kampuni ya LG kwa kushirikiana na kampuni hiyo.
Wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka kubwa la bidhaa za kieletronic kwa mara ya kwanza Arusha.
Mr Nyoung Kim Mkurugenzi Kampuni ya LG akiashiria ufunguaji wa duka hilo mara baada ya zoezi la kukata utepe kukamilia.
Picha ya Pamoja wadau wa kampuni ya LG  .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...