Kamanda wa Polisi mkoani hapo ACP Benjamin Kuzaga akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 2,2021.

Na John Walter-Manyara
JESHI la Polisi mkoani Manyara katika opereshi mkoani humo limewakamata watu wanne kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Bangi Misokoto 25 na Mirungi Bunda 48.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani hapo ACP Benjamin Kuzaga imeeleza kuwa Novemba 29,2021 huko eneo la Maramboi kijiji cha Minjingu kata ya Nkaiti tarafa ya Mbugwe wilaya Babati, walimkamata Omary Fadhili (26) mkazi wa Bonga akiwa anaendesha pikipiki yenye namba MC 986 CZW akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Mirungi Bunda 41 yenye uzito wa kilo 20 ikiwa imefungwa kwa kutumia gazeti na kuwekwa kwenye boksi la rangi ya kaki kisha kufunga katika pikipiki.

Kamanda Kuzaga amesema wanamshikilia Halima Mandi (49) mkazi wa Unga Limited jijini Arusha akiwa na Mirungi bunda saba sawa na kilo 2.92 yakiwa yamehifadhiwa kwenye pochi aliyokuwa ameibeba akiwa ndani ya basi kampuni ya Zakaria Express lenye namba T349 AGN linalofanya safari zake Arusha-Kiteto.

Mwanamke huyo alikamatwa Novemba 30 mwaka huu njia panda ya Kijiji cha Njoro kata ya Njoro tarafa ya Olboloti wilaya ya Kiteto.

Aidha jeshi hilo katika kijiji cha Magugu eneo la kituo cha Mabasi waliwakamata Haiba Ally (45) na Zuhura Bashir (22) wote wakazi wa Magugu kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi.

Kamanda Kuzaga amesema Haiba Ally alikutwa na bangi misokoto mitano sawa na gramu 0.85 akiwa ameifunga kwenye kitambaa chekundu na kuiweka katika mfuko wa nyuma wa suruali ya jinsi aliyokuwa ameivaa.

Pia amesema mtuhumiwa Zuhura Bashir alikutwa na misokoto 20 sawa na gram 150 akiwa amehifadhi ndani ya friji lililokuwa kwenye chumba anacholala.

Amesema watuhumiwa wote wanne watafikishwa mahakamani pindi ushahidi utakapokamilika kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...