Kasulu, Kigoma
WAUZAJI wa Rejareja wa pembejeo za kilimo za Kampuni ya Mbolea ya Yara wametakiwa kuitumia kikamilifu programu ya yaraConnect ili sio tu kujipatia zawadi bali kunufaika na elimu kuhusu matumizi sahihi ya pembejeo hizo.
Wito huo aliutoa Meneja Masuluhishi ya Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei mjini Kasulu, Mkoani Kigoma jana, katika hafla ya kutoa zawadi ya pikipiki kwa mmoja wa wauzaji wa pembejeo za Yara Bwana Yotham Mbwila Tanditse wa Kampuni ya Mbwila Mbwila General Supplies, aliyefanikiwa kufikia vigezo vilivyowekwa.
Alisema programu ya yaraConnect ilizinduliwa Julai 1 mwaka huu ikiwa na lengo la kutoa msaada wa utaalamu wa kilimo na matumizi Bora ya Mbolea za Yara hivyo wauzaji hupata nafasi ya kujifunza na kupata majibu ya maswali yanayohusiana na kilimo pamoja na matumizi sahihi ya pembejeo za Yara.
“Ndani ya yaraConnect kuna sehemu tunaita video za maarifa ambapo muuzaji atapata madodoso kwa maandishi ama video Kuhusu mlipuko wa magonjwa au shida yoyote ya kilimo iliyotokea hivyo kuweza kutoa taarifa hizo kwa wakulima”, alisema.
Alisema ndani ya yaraConnect pia Kuna sehemu ya msaada ambapo muuzaji anaweza kuwasiliana moja kwa moja na kitengo Cha huduma kwa wateja kuhusu Jambo lolote Kama upatikanaji wa bidhaa za Yara, bei au masuala mengine yanayohusiana na pembejeo za Yara.
“Kingine kikubwa ni kuwa hivi karibuni tutaleta mfumo ambao wakulima watakuwa na nafasi ya kuweza kujua maduka ya pembejeo zetu yaliyo Karibu na wao hivyo kwa kujisajili katika programu ya yaraConnect mfanyabiashara atapata nafasi ya kujitangaza bure kwa wakulima walio katika eneo lake”, aliongeza Bwana Mtei.
Bwana Mtei alisema ili kujiunga na programu ya yaraConnect muuzaji alitakiwa kuipakua mtandaoni kupitia simu janja kupitia Google play store kwa watumiaji wa Android ama app store kwa watumiaji wa iPhone kusajili biashara zao na kujipatia pointi zinazowawezesha kupata zawadi mbalimbali ikiwepo pesa taslimu, simu ya mkononi na zawadi kubwa ya pikipiki.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake mshindi huyo Bwana Yotham pamoja na mkewe Bi. Oliver, waliwahamasisha wafanyabiashara wa Mbolea wilayani kasulu kutumia yaraConnect ili waweze kupata maarifa ya kilimo na pia kujishindia zawadi kwani ni za kweli.
Meneja Masuluhishi ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Deodath Mtei, baadhi ya wafanyakazi wa Yara wakimpongeza muuzaji bora wa pembejeo za Yara kwa kutumia programu ya yaraConnect, Yotham Mbwila Tanditse (wa tatu kushoto), baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki katika hafla iliyofanyika wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...