Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kuanza kutoa faida kwa wateja wa Airtel Money, Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda, alisema, “tuna furaha kubwa sana kuona kuwa huduma ya Airtel Money inaendelea kuwa msingi wa shughuli za kibiashara hapa nchini. Tuko katika mchakato wa kugawa Shilingi bilioni 2,011,886,007 kwa wateja wetu ambao wamekuwa wakitumia mfumo wetu kwa kipindi hiki, na malipo yanaingia moja kwa moja katika akaunti zao za Airtel Money.”
Faida italipwa kwa wateja, mawakala, wakala mkuu na wadau wengine wa kibiashara wa Airtel Money kulingana na matumizi yao ya huduma za Airtel Money. Faida linategemea kiasi cha matumizi ya huduma katika kipindi hicho cha Julai mpaka Septemba 2021. Shughuli hizo ni pamoja na kuhamisha pesa, kulipa bili, manunuzi ya muda wa maongezi na mengine.
Mara baada ya kupokea faida yake, wateja wa Airtel Money wanaweza kutumia faida hilo kwa njia ya kutoa pesa taslimu, kununua vifurushi vya maongezi na data au kutumia kulipia bili au manunuzi ya bidhaa.
Nchunda aliongeza, “Mfumo huu wa kipekee umekuwa na nafasi kubwa katika kujenga hali ya ushirikishwaji na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Wanawake na vijana wameona unafuu na urahisi wa kutumia Airtel Money na wanatumia huduma nyingi ili kuboresha maisha yao. Pia mfumo umekuwa rasilmali muhimu katika kuwezesha biashara ndogo ndogo. Kwetu Airtel Tanzania, dhamira yetu ni kuhakikisha kuwa mfumo huu unaendelea kuwa mfumo unaoendana zaidi na mahitaji ya wateja.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...