Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WAANDISHI wa habari watano kutoka mbalimbali vya habari nchini wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali mkoani Mwanza.
Waandishi hao ambao wameripotiwa kufariki dunia ni Abel Ngapemba ambaye ni Ofisa Habari Mkoa wa Mwanza, Johari Shani wa Uhuru Media Group, Husna Mlanzi na Athony Chuwa wanatoka ITV pamoja na Steven ambaye Ofisa Habari Wilaya ya Ukerewe na Majeruhi ni Tunu Heman - Freelancer na Vany Charles - Icon TV
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimeifikia Michuzi TV na Michuzi Blog ni kwamba Waandishi hao walikuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye alikuwa akielekea wilayani Ukerewe kwa ziara ya kikazi .Gari waliyokuwamo waandishi hao ilipata ajali baada ya kugongana na gari aina ya Hiace.
Mwekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza Edwin Soko kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema ajali hiyo imetokeaa eneo la Busega na Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza amethibitisha vifo vya watu watano."Nawaomba tuwe watulivu kwa wakati huu."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...