Bodi ya Wakurugenzi ya Pan African Leadership and Entrepreneurship Centre (PALEDEC) imemtangaza Mheshimiwa Balozi wa Visiwa vya Shelisheli Maryvonne Pool kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kuanzia Januari 10 mwaka huu Hadi ifikapo mwaka 2024.
Kabla ya uteuzi huo Mheshimiwa Maryvonne alishinda tuzo ya heshima inayotambua mchango wa maisha yake katika kutoa misaada ya kiutu wakati wa Mkutano wa sita wa (Pan African Humanitarian Summit and Awards) uliofanyika Novemba, 2021 Jijini Istanbul nchini Uturuki
Alipata tunzo hiyo kutokana na mchango wake katika kujitolea kwenye kazi za uwezeshaji kwa wanawake kiuchumi na kukuza maendeleo ya vijijini.
Maryvonne ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalofahamika kwa jina la African Reflections Foundation ambalo limejikita zaidi katika kuboresha upatikanaji wa elimu bora, maji safi na salama na kwa uhakika, kuwawezesha wanawake kiuchumi, utoaji wa huduma katika sekta ya afya na uboreshaji wa vituo na kukuza maendeleo vijijini kupitia viwanda vidogo na vya kati vinavyoongeza thamani ya mazao ya kilimo.
“Nimefurahi kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Kituo cha Maendeleo ya Uongozi na Ujasiriamali cha Pan African (PALEDEC) nimekuwa nikipendezwa na ukuaji endelevu wa Afrika kwa ujumla na ninatarajia kufanya kazi na PALEDEC na washirika kubadilisha uwekezaji endelevu na kukuza uchumi wa buluu' .
Balozi MaryVonnre alisema kuwa vodi ya PALEDEC ina jukumu muhimu katika kuongoza ushirikiano na kuhakikisha kuwa uwekezaji wa ndani ya Bara la Afrika unakuwa kitovu cha uchumi na kuwa ajenda ya kikanda na kimataifa ili kuimarisha maendeleo ya watu, kwa usawa na endelevu Barani Afrika.
"Kamati ya Bodi na mimi tutaendelea kujenga ushirikiano imara na viongozi katika Jumuiya za Diaspora na Afrika ili kupunguza umaskini katika bara hili na kufikia maendeleo endelevu." alisema Balozi huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...