Mwamvua Mwinyi,Pwani.

Kero ya muda mrefu ya ukosefu wa daraja kwa Wananchi wa kata ya Mbuchi Wilayani Kibiti ,Mkoani Pwani inakwenda kubaki historia baada ya Ujenzi wa Daraja linalounganisha kata ya Mbuchi na Bwera lililogharimu sh.Bilioni 6 .2 kukamilika kwa asilimia 80.

Baadhi ya wakazi hao wameishukuru serikali kwa ujenzi wa daraja hilo na kusema walitaabika kwa kipindi kirefu, huku wajawazito wakipata changamoto wakiwa wanaenda kujifungua.

Hamis Iddi, Shahaa Baruani na Mhidin Mwinyihaji walieleza, pia walikuwa na kero katika kuvuka mto na kusafirisha mazao kutoka mashambani kwa kutumia mtumbwi.

Iddi aliishukuru Serikali na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwaondolea adha ya usafiri kwa kuwajengea Daraja Hilo linalounganisha kata ya Mbuchi na Bwela kwani wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu .

"Hakika daraja limekuwa mkombozi kwani ilifika wakati wa kusafirisha mazao toka shambani tunatumia gharama kubwa kuvusha katika mto kwa kutumia mtumbwi."

Akitembelea na kukagua Daraja hilo, mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alibainisha, amefika kujionea hatua zilizofikia katika ujenzi huo .

,"Tunamshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwatumikia watanzania,

Hivyo kutokana na kukamilika kwa daraja hili ,wananchi mtaweza kupata fursa ya ajira na kuvuka salama"alifafanua Kunenge.

Awali akisoma taarifa kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Meneja wa Wakala wa Barabara za vijijini na mijini -TARURA mkoa wa Pwani ,mhandisi Leopold Runji anasema mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 6 .2 .

Runji alisema, daraja hilo lina urefu wa mita 61 na linatarajiwa kuanza kutumika tarehe 23 mwezi January mwaka huu 2022.

Nae diwani wa kata ya Mbuchi ,Yusuph Mpili alisema kwamba, kutokana na daraja hilo matatizo yote yanakwenda kupungua na kuisha ikiwemo suala la akina mama wajawazito kupata shida wakati wa kwenda kujifungua.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...