Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini mkoa wa Dar es Salaam (TARURA), Mhandisi Geofrey Mkinga akizungumza na Mwandishi wa Michuzi blog hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.


* Faini ya shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja
*Sheria ya barabara hairuhusu kufanya biashara maeneo ya barabara

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
KUFANYABIASHARA kwenye maeneo barabara kunachelewesha maendeleo ya kila mmoja pamoja na kupunguza spidi ya magari yawapo barabarani.

Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini mkoa wa Dar es Salaam (TARURA), Mhandisi Geofrey Mkinga amesema hayo wakati akizungumza na Michuzi blog jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kufanya biashara kwenye hifadhi ya barabara ni kinyume cha sheria ya barabara ya mwaka 2007.

Akielezea maana ya hifadhi ya Barabara anasema kuwa ni eneo lote kuanzia katikati ya barabara mpaka kwenye eneo ambalo ni la viwanja vya watu kwa upande wa kulia na kushoto mpaka mipaka ya kiwanja cha mtu kinapoanzia.

Mhandisi Mkinga anasema kuwa Kweye Sheria ya Barabara ya Mwaka 2007 Sheria Namba 13, Kifungu Namba 29 hifadhi ya barabara ndani yake inaweza kupitishwa miundombinu mingine miundombinu hiyo ni ya umeme, ya simu, majisafi na majitaka, miundombinu ya gesi, miundombinu ya mabango ya matangazo na mitaro ya majitaka.

Pia amesema pembeni yake kunaweza kutengenezwa maegesho ya magari pamoja na kutengeneza bustani ambazo hutengenezwa kwa kibali maaalumu cha mwaka mmoja kutoka TARURA na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

Licha kwa kuwepo kwa wafanyabiashara katika hifadhi ya barabara lakini iwapo mamlaka husika itahitaji eneo hilo mfanyabiashara lazima aondoke mara moja bila kulipa fidia yeyote.

Amesema kuwa kwa sasa vibali hivyo vimesitishwa kutolewa kwa sasa kwaajili ya kupisha uondoshaji wa wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katika maeneo ya hifadhi za barabara bila kuwa na kibali licha ya kuwa walikuwa wakijipatia riziki.

Mhandisi Mkinga amesema sheria ya barabara ya mwaka 2007 sheria namba 13, kifungu namba 50 kifungu kidogo cha 2 (i) kinaruhusu mtu anayevunja sheria ya barabara na hifadhi barabara kupigwa faini ya shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja.

Akielezea umuhimu wa Hifadhi ya barabara Mhandisi Mkinga amesema kuwa hifadhi ya barabara inaachwa kwaajili ya matumizi mengine pamoja na upanuzi wa barabara pale yanapohitajika kulingana na maendeleo ya eneo husika.

Amesema kuwa Machinga waliondolewa kwa mujibu wa sheria ya baraba ya mwaka 2007 sheria namba 13 kifungu namba 50 kwasababu wafanyabiashara hao wanazuia watu wengine kutembea, kuzuia magari kwenda kwa spidi inayotakiwa sababu walikuwa wakipanga biashara zao hadi sehemu za watembea kwa miguu na kusabisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan aliamuru wafanyabiashara ndogondogo wapangwe vizuri na wafanyie biashara kwenye maeneo ambayo yanaruhusiwa kufanya biashara.

Amesema athari zilizokuwa zikijitokeza kwa wafanyabiashara kufanya biashara katika maeneo ya hifadhi ya barabara ni kupoteza maisha pamoja na mali zao, kusababisha msongamano wa watu na msongamano wa magari katika maeneo hifadhi za barabara zilizovamiwa na wafanyabiashara.

“Tunataka watu wakatumie zaidi maeneo yaliyopangwa kwaajili ya kufanyia biashara na serikali yetu imejitahidi sana kutafuta maeneo ya kufanyia biashara, watu wakatumie maeneo hayo tunasisitiza.” Anasisitiza Mhandisi Mkinga.

Kwa upande wake Dereva wa Daladala la kutoka simu 2000 hadi Mbezi, Gastoni Mwenda amesema kuwa kuwaondoa wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara pembezoni mwa barabara ni jambo linalowaumiza lakini kwa upande, lakini kumekuwa hakuna kusimama simama kwa gari pale watu wanapokuwa kwenye msongamano hasa wakiwa wananunua bidhaa zao.

“Kwa kiasi fulani Kimara palikuwa na msongamano wa magari kwa sababu wafanyabiashara waliokuwa wakisababisha madereva tuendeshe magari kwa uangalifu sana ili tusiwagonge watu ambapo ni tofauti na sasa palivyo.” Amesema Mwenda

Akizungumzia juu ya kujua sheria za hifadhi za barabara Mafanyabiashara wa mama Ntilie wa Kituo cha Morroco jijini Dar es Salaam, Anna Siwa amesema kuwa “sheria zimewekwa ili zivunjwe ni kweli kunasheria lakini sio kila mtu anazijua.” Hivyo tunaomba serikali pamoja na vyombo vinavyohusika kutoa elimu juu ya suala la sheria za barabara na hifadhi za barabara kwa kila manyabiashara aliyekuwa akifanya biashara kwenye hifadhi ya barabara anajiona alikuwa na haki kuanya.

“Kwa upande wangu naona waliokuwa wanafanyabiashara juu ya mitaro kwa walikuwa hawapo sahihi maana matakataka yake sidhani kama alikuwa akihifadhi sehemu ya kuhifadhia taka, mtaro utakuwa ulikuwa ndio kitunzio chake, na hiyo inakuja kusumbua mvua zikinyesha maji yanakuwa hayapiti.” Amesema Anna.
Moja ya mabango yaliyowekwa na Manispaa ili kuzuia wafanyabiashara katika maeneo ya hifadhi za barabara katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...