Na Khadija Seif, Michuzi tv
SHIRIKA la Haki za bidamu (LHRC) Kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) limetambulisha rasmi Mradi wa Majaribio unaolenga kuzuia na kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wa kingono.
Akizungumza na waandishi Wahabari jijini Dar es salaam wakati wa kutambulisha Mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Anna Henga amesema Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na kituo cha sheria na Haki za bidamu (LHRC) Kwa mwaka 2019/2021 ilibainika kuwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kingono katika Wilaya ya Kinondoni vimeongezeka.
"Tulibaini Kuna matukio 57,626 na kati ya hayo mengi yalikuwa udhalilishaji na ukatili wa kijinsia hasa udhalilishaji wa kingono Kwa mwaka 2019/2021.
Aidha ,Henga amefafanua zaidi na kusema kuwa vitendo hivyo viliwaathiri sana makundi maalum ikiwemo watoto,watu wenye ulemavu na wanawake.
"Kutokana na kuwepo Kwa janga la ugonjwa wa uviko 19 Kwa mwaka 2020 na Kwa upande wa watoto,janga hili liliilazimu Serikali kufunga shule na watoto kurudi nyumbani Kwa takribani miezi mitatu na katika kipindi hicho watoto walikuwa nyumbani kuliripotiwa kuongezeka Kwa matukio ya ukatili dhidi Yao hasa ukatili wa kingono na mimba za utotoni."
Aidha Henga amesema lengo la Mradi huo wa Majaribio una lengo la kujenga uwezo na kuhamasisha wadau mbalimbali Ili kuweza kuzuia na kukabiliana na changamoto za matukio ya udhalilishaji wa kingono kwa makundi mbalimbali.
"Tutafanya tathmini ya jinsi ya kuandaa program za udhalilishaji na unyanyasaji wa kingono zenye tija na ufanisi na Kwa Sasa Mradi huo unatekelezwa katika Hospitali ya Mwananyamala".
Kwa upande wa Mratibu wa Huduma ya Mkono kwa Mkono Kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala Asia Mkini amesema kutokana na usumbufu wanaopata waliopata kadhia hiyo ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hususani waliobakwa kupata haki zao Kwa haraka zaidi hivyo Kwa kupitia Huduma ya Mkono kwa Mkono inayotolewa hospitali ya Mwananyamala imewezesha upatikanaji wa hatua za awali zote kuwekwa sehemu Moja.
"Huduma ya Mkono kwa Mkono imeanzishwa rasmi Ili kuweza kurahisisha Huduma za awali kufanyika Kwa haraka Ili kupunguza ucheleweshwaji wa Majibu kutoka polisi na Hospitali."
Hata hivyo ametoa tathmini jinsi ya kesi ambazo zimeshiriki katika Huduma ya Mkono kwa Mkono nakufikia takribani kesi 100 na Kwa upande wa watoto ni 84% kuliko kesi za watu wazima.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na Haki za bidamu (LHRC) Anna Henga akitambulisha Mradi wa Majaribio unaolenga kuzuia na kukabiliana na changamoto za matukio ya udhalilishaji na unyanyasaji wa kingono.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...