Adeladius  Makwega,Moshi

Mangi Mkuu wa Wachaga Frank Mareale amesema kuwa maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la Kilimanjaro yanaendekea huku wakishirikiana kwa karibu na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mkoa wa Kilimanjaro, Machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro na wadau mbalimbali ambalo linatarajiwa kufanyika Januari 22, 2022 katika Viwanja vya Chuo cha Ushirikia Moshi tangu saa moja asubuhi.

Akizungumzia maandalizi hayo Chifu Mareale amesema kuwa mpaka sasa wamehakikishiwa kuwa Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani, huku wageni wengine kadhaa wakiwamo machifu kumi wanaoziwakilisha kanda zao , viongozi kadhaa wa dini na wananchi wa Mji wa Moshi watashiriki.

“Naomba wakaazi wote wa Moshi na viunga vyake wajitokeze katika tamasha hili, maana utamaduni ni mali ya watu si mali ya Mangi pekee, nawaomba waje kuona mila na tamaduni zetu.”Alisema Chifu Mareale. 

Akizungumza katika kikao cha kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Mkurugenzi wa Utamaduni Nchini Dkt Emmanuel Temu amesema kuwa kwa hakika maandalizi yanaendelea vizuri huku kukiwa na ukaguzi wa kiwanja kitakachotumiwa kwa tamasha hilo na vikundi vya hamasa na burudiani.

“Sisi kama wizara husika, tupo na tunafuatlia kila hatua ya maandalizi hayo, kuhakikisha tamasha hili linafanikiwa na kufana.”Alisisitiza Dkt Temu.

Tamasha hilo linapambwa chini ya kauli mbiu ya “Utamaduni wetu, fahari yetu, kwa maendeleo yetu- Kazi iendelee.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...