Adeladius Makwega,Dodoma.
Rail On.
Hayo uliyosoma ni mashairi ya Wimbo Rail On (machozi) wa Jules Shungu Wembedio Pene Kikumba(Papa Wemba) mwanamuziki aliyekuwa na asili ya Kongo ambaye alikuwa akicheza muziki wa Rumba, Soukus na Ndombolo.
Wimbo huu una maneno 102 huku maneno Rail On pekee yakijirudia mara 20 kwa 20 kwa hiyo maneno 62 ndiyo yalitumia lugha ya Kiswahili. Ninaweza kusema wimbo huu umeimbwa Kiswahili kwa msingi wa maneno mengi yalitumika dhidi ya maneno ya kimombo.
Siku ya jana niliukumbuka wimbo huo ambapo unazungumzia mapenzi wa kiume ambaye analalamika kuondoka kwa mpenziwe wa kike, mtunzi hakueeleza kuwa kama mpenzi wake wa kike amemuacha kwa kwenda kwa bwana mwingine ama ameondoka duniani.
Lakini mkomonzio wa wimbo huo unajengwa katika huzuni kubwa ya mpenzi wa kiume kwa kilio hicho. Muziki unaweza kujengwa katika maneno ukatoa taswira ya wimbo,una weza ukajengwa katika vyombo tu ukaonesha taswira yake na pia hata sura ya yule anayeimba inaweza kuonesha taswira ya wimbo huo.
Leo hii mwanakwetu
naweka kalamu chini hapo, nikikumbusha kuwa Aprili 24, 2022, itakuwa imetimia
miaka 6 tangu Papa Wemba afariki dunia.Ndugu huyu ana nyimbo tele kama vile
Yolele, Mandola, Show me the way, Shofele na nyingine nyingi.Nakutakiwa siku
njema.
0717649257
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...