Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAMIA ya wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi katika Wiki ya utoaji elimu kwa wafanyabiashara iliyaondaliwa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA).

Katika utoaji huo wa elimu ambao unakwenda sambamba na kuwahudumia wananchi ambao wanahitaji kusajili majina ya biashara pamoja na kampuni wameamua kuja na kampeni inayosema Kamilika 2022 wakiwa na maana huu ni mwaka wa mfanyabiashara kukamilisha kila kitu.

Akizungumza na Michuzi TV leo Januari 29,2022 ,Msaidizi wa Usajili wa BRELA Vyonne Masele tangu wameanza kutoa huduma hiyo katika Viwanja vya Mliman City , muamko umekuwa mkubwa na mkakati wa Wakala huo ni kuhakikisha wafanyabishara wanarasimisha biashara zao.


Amefafanua kuwa kupitia kampeni hiyo ya kutoa elimu na huduma , wanatamani kuona wafanyabishara wanakuwa wamekamilika kwa kufuata tararibu zote za kisheria ikiwa pamoja na kuwa na leseni, "Lengo letu tunataka wafanyabiashara wawe wamekamilika, wamesajili kampuni, wamepata leseni na wamerasimisha biashara zao."

Alipoulizwa ni mambo gani ambayo wanaofika kuhudumiwa wanapenda kuyafahamu kutoka BRELA,Vyonne Masele amesema wengi tangu wameanza kampeni wengi wanafika kusajili majina ya biashara , kusajili kampuni lakini wengi pia wanataka kujua mambo gani ya kufanya ili kupata majina ya kampuni na leseni pamoja na kuingia kwenye mfumo wao ili kujaza fomu.

"Kiukweli kwenye kufungua akaunti kwa mteja sio ngumu ,sema wanachokihitaji ni kueleweshwa mara kwa mara ili kuzoea namna ya kuingia kwenye mfumo wetu.Kwa mfano mtu aaweza kutmiwa E-Mail ili kuendelea na mchakato wa usajili lakini unakuta hawafungui zile e-mail."

Masele ametoa mwito kwa wananchi kufika maeneo hayo ambayo BRELA wameamua kufanya kampeni hiyo ili waweze kuhudumiwa ikiwa pamoja na kupata majina ya biashara na kusajili kampuni kwani bado kuna wafanyabishara ambao wanatumia majina katika biashara zao lakini hayajasajiliwa, hivyo ni vema wakafika kuhudumiwa.

Maofisa wa BRELA wakitoa Huduma kwa wananchi waliofika katika Viwanja vya Mliman City mkoani Dar es Salaam.BRELA wako katika Wiki ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kurasimisha biashara zao na masuala mengine katika biashara



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...