KATIKA Muendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza sekta ya utalii nchini.

Mbunifu nguli nchini Tanzania Mustafa Hassanali, anatarajiwa kushiriki onyesho la ubunifu wa mavazi yenye dhima ya safari.

Dhumuni la jukwaa hili la Mavazi kubuniwa  ni kushawishi watalii kununua nguo zao za Safari nchini Tanzania akiwa na nia ya kutangaza nchi na kukuza sekta ya utalii nchini Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika Januari 29 mwaka huu, mkoani Manyara Mawemawe, hii itakuwa baada ya miaka saba ya kutokuonyesha mavazi yake nchini Tanzania.

"Mama amefungua njia kwa kutuonyesha fursa katika sekta ya utalii na mimi kama mbunifu niko tayari kutoa ushirikiano katika kufanikisha kutangaza nchi hivyo tutauza nguo za safari kwa watalii" amesema Mustafa Hassanali.

Tukiwa tunasubiri Royal Tour ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tunapenda kuchukua nafasi kushukuru viongozi wa Mkoa wa Manyara kuanzia mkuu wa mkoa Bwana Makongoro Nyerere kwa kutunza na kuenzi mbuga zilizopo mkoani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...