Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) imeendelea kutoa
elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za
Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli
mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya uhasibu.
Akizungumza
wakati wa kutoa mafunzo hayo Afisa wa NBAA kutoka Idara ya Elimu na
Mafunzo, Ibrahim Magambo amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza
kufanya kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili
kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza
kufanya kazi nje na ndani ya nchi.
Aliongeza
kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu
nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya
ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya
Uhasibu na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza
kufanya mitihani ya Bodi alisema Magambo
Naye
Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Modest Assenga
ameishukuru Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA)
kwa kuweza kufika kwenye Taasisi hiyo na kutoa elimu kwani baada ya
wanafunzi hao kumaliza masoma yao itakuwa rahisi kuweza kujiunga na
mitihani ya Bodi kwa kuwa watakuwa na uelewa kuhusu Bodi hiyo pamoja na
CPA.
Afisa
wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kutoka
Idara ya Elimu na Mafunzo, Ibrahim Magambo akitoa elimu kwa wanafunzi
wanaosoma masomo ya Uhasibu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)
iliyopo Dar es Salaam ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu kazi
zinazofanywa na Bodi hiyo kwa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za
Sekondari.
Afisa
Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya(katikati) akitoa ufafanuzi
kuhusu kazi zinazofanywa na bodi hiyo wakati wa mafunzo kwa Wanafunzi
wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yalifanyika katika ukumbi wa
Taasisi hiyo iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri
wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Modest Assenga akitoa neno
kwa shukrani kwa wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi
Hesabu Tanzania(NBAA) waliofika katika chuo hicho kwa ajili ya kutoa
elimu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Uhasibu kuhusu kazi zinazofanywa
na Bodi ya NBAA.
Baadhi
ya wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakifuatilia mada
kutoka ka maofisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu
Tanzania(NBAA) waliofika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu
kazi zinazofanywa na Bodi hiyo pamoja na namna ya kuweza kupata CPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...