Na Said Mwishehe, Michuzi TV
UCHUKUAJI wa fomu za kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina zidi kushika kasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Kada wa Chama hicho Joseph Elias Sabuka ni miongoni mwa makada waliochukua fomu hiyo.
Kada huyo amechukua fomu katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, leo Januari 13,2022 , ambapo ameeleza kuwa amejitathimini na kuona ana uwezo na Sifa za kuongoza mhimili huo.
“Uzoefu nilio nao ndiyo utakaonivusha katika mchakato huu kumpata spika. Nikichaguliwa kuwa spika kitakachoniongoza ni sheria kanuni na miongozo. Nitakuwa imara kuisimamia na kuhakikisha siyumbi.Nitaisamimia Serikali na kuikosoa pale kwenye ulazima wa kufanya hivyo,” amesema Sabuka.
Kada huyo, ambaye ni Ofisa Mwandamizi katika Serikali ya Awamu ya Sita anayehudumu katika Wizara ya Fedha na Mipango mesema haoni kama kuna shida kwake kugombea nafasi hiyo kwani uzoefu alio nao katika kutekeleza majukumu ya Chama na serikali ndiyo utakaomvusha katika mchakato huo.
“Ni meamua kugombea kwani ni haki yangu kikatiba, demokrasia , nina sifa, uwezo na nia”amebainisha”.
Ameleeza mwaka 2020 aliwahi kuomba ridhaa ya Chama kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kinondoni mkoani Dar es Salaam lakini kura hazikutosha na sasa ameona ni wakati sahihi kwake kuomba kuwania nafasi ya Spika wa Bunge.
Amezungumzia pia mfumo wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ndani ya CCM ambapo ametoa pongezi kwa chama chake kwan namna ambavyo utaratibu uliowekwa ni rafiki na wa kidemorasia.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...