Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Jeshi
la polisi makao makuu limefanya uzinduzi wa matumizi ya mashine mpya za
malipo kwa ajili kukusanya maduhuli ya serikali katika mkoa wa kipolisi
Rufiji kwa kamanda wa polisi,mafisa,askari wa usalama barabarani pamoja
na wahasibu.
Lengo
la mashine hizo mpya zenye uwezo mkubwa Sambamba na mafunzo ni
kuwajengea uwezo wa kutoa huduma kwa muda mfupi na kuondoa malalamiko
yaliyokuwa yakijitokeza kipindi cha nyuma.
Hayo
yalisemwa na Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Leonard Ngassa
alipofanya ziara katika mkoa wa kipolisi Rufiji ,kutoa elimu kwa askari
juu ya matumizi ya mashine mpya za kukusanya maduhuli ya serikali.
Alieleza,
mashine hizi zitakuwa na uwezo mkubwa tofauti na awali kwani
zimeongezewa baadhi ya mifumo ili kutoa huduma kwa haraka.
"Nia
ya ziara yetu ni kutoa elimu na uzinduzi wa matumizi ya mashine
hizi,Tunaishukuru Serikali kwa kuliwezesha Jeshi la polisi kwa ajili ya
ununuzi wa mashine hizo, Tutaanza kutoa mafunzo nchi nzima kwa makamanda
wa polisi,askari wa usalama barabarani, maafisa,wakaguzi na wahasibu"
alifafanua Leonard Ngassa-Kamishna msaidizi wa polisi kutoka makao
makuu.
Nae
Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi na Kamanda wa polisi mkoa wa
kipolisi Rufiji ,Kungu Malulu alisema mashine hizo zitaongeza ufanisi wa
kazi kwa askari pamoja huduma bora kwa wananchi wa mkoa wa kipolisi
Ruiji.
"Tumepokea ugeni kutoka makao makuu kwa Ajili ya askari wetu ambapo pia tumepokea mashine hizi za kisasa"
Malulu
alibainisha,kwa hakika ujaji wa mashine hizo utaboresha utoaji huduma
na kuongezea ufanisi wa kazi kwa askari Rufiji na maeneo mengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...