Na Humphrey Shao, Michuzi Tv.


Ikiwa kesho Ni Jumamos ya mwisho wa Mwezi ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam umetenga siku hiyo kwaajili ya Usafi wa pamoja, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amos Makalla  anataraji kufanya usafi katika eneo la Manzese Wilaya ya Ubungo ikiwa na iMwendelezo wa kampeni ya Safisha , Pendezesha Dar es Salaam.

RC Makalla ametoa wito huo wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya Usafi kwa Shule zote za Mkoa huo ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es salaam ambapo amesema kwa siku ya kesho zoezi la Usafi kimkoa litafanyika Wilaya ya Ubungo eneo la Manzese na Wilaya nyingine zitaratibu Usafi kwenye maeneo yao kuanzia ngazi ya Mtaa hadi kata.


Aidha RC Makalla ameelekeza Maafisa Elimu kuandika waraka wa kuelekeza kila Shule kufanya Usafi na kupanda Miti ili Kupendezesha Mandahari ya Jiji.


Hata hivyo RC Makalla amesema Kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es salaam Ni endelevu hivyo ametoa wito kwa Wananchi kuzingatia Usafi kwenye maeneo yao.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa , Amos Gabrile Makalla akizungumza na Walimu pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Zanaki Jijini Dar es Salaam.


Mmoja ya Watendaji wa NMB Akikabidhi Kapu la kuwekea taka lililotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kusaidia kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Amos Makalla akikabidhi vifaa vya usafi kwa mwalimu Mkuu wa Gerezani Sekondari kama ishara ya kugawa kwa shule zote.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Zanaki.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...