Na. Damian Kunambi, Njombe
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amewata viongozi wote wa ngazi ya wilaya na kataka katika mkoa wa Njombe kuweka azimio la kupiga marufuku uaandaaji mashamba kwa kuchoma moto ili kutunza mazingira pamoja na ubora wa ardhi.
Tsere ameyasema hayo alipomuwakilisha mkuu wa mkoa huo Mhandisi Marwa Rubirya katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti liliilofanyika katika wilaya ya Ludewa kata ya Lubonde kijiji cha Kiyombo.
Amesema wakulima wengi wamekuwa wakichoma moto masalia ya shambani kitu ambacho huaribu rutuba ya ardhi bali wanapaswa kukusanya masalia hayo na kuyafukia pembeni ambapo kwa kufanya hivyo hutengeneza mbolea aina ya Mboji.
Ameongeza kuwa mkoa huo unaongoza kwa matumizi ya mbolea katika mazao kwakuwa ardhi yake huaribiwa kwa kuchoma moto kitu ambacho hupelekea udongo kutokuwa na rutuba ya kutosha.
"Endapo tutaacha tabia ya kusafisha mashamba kwa kuchoma moto tutaokoa ardi zetu, uharibifu wa vyanzo vya maji, uharibifu wa miti iliyopandwa na ya asili pamoja na kuokoa viumbe hai vinavyoishi maporini", Amesema Tsere.
Aidha katika zoezi hilo la upandaji miti mkuu huyo amesema ni utekelezaji wa sera ya serikali ambayo inawataka kupanda miti Ml.1.5 kwa kila Halmashauri hapa nchini ambapo kwa mkoa wa Njombe katika mwaka 2021 tayari ulishapanda miti zaidi ya Ml. 40 ikiwa na wastani wa zaidi ya miti Ml. 5 kwa halmashauri sita za mkoa huo hivyo katika mwaka 2022 wanatarajia kupanda miti zaidi ya Ml. 25.
Amesema miti hiyo hupandwa kwaajili ya kukuza uchumi na kunufaisha jamii ambapo itazalisha mbao kwa wingi, milingoti na mazao yote yanayotokana na miti ikiwemo kuni.
Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya Lubonde Edga Mtitu amesema ili kupunguza majanga ya moto wakazi wanaozunguka misitu hiyo wanapaswa kuwa walinzi wa misitu hiyo hivyo serikali inapaswa kutoweka masharti magumu ya kufanya shughuli mbalimbali katika misitu hiyo ikiwemo kuokota kuni.
"Katika miaka ya nyuma masuala ya uchomaji moto hayakuwepo kwa wingi kwakuwa wakazi wa maeneo hayo walikuwa wanashirikishwa katika shughuli mbalimbali zinazohusu misitu, walikuwa wanapata ajira mbalimbali na walikuwa wanaruhusiwa kuokota kuni, lakini baada ya serikali kuweka masharti magumu kwa wananchi misitu imekuwa ikiungua kwakuwa haina ulinzi", amesema Mtitu.
Katika zoezi hili la upandaji miti kwa mwaka huu limeambatana na kauli mbiu inayosema MITI, MAZINGIRA YANGU,TANZANIA YANGU NAIPENDA DAIMA.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere akipanda mti katika kata ya Lubonde kijiji cha Kiyombo akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere (kushoto) akisoma risala ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti mkoa wa Njombe kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Mhandisi Marwa Rubirya. Kulia kwake ni mkuu wa Polisi wilaya ya Ludewa Deogratius Masawe
Mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya ya Ludwa Wise Mgina akipanda mti katika kata ya Lubonde kijiji cha Kiyombo ikiwa ni uzinduzi wa zoezi la upandaji miti mkoani Njombe.
Mkuu wa polisi wilaya ya Ludewa Deogratius Masawe akipanda mti katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti mkoa wa Njombe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...