Na.Khadija Seif, Michuziblog
WAKONGWE wa Tasnia ya Ubunifu wa Mavazi nchini wanatarajiwa kushiriki katika Onyesho la Wiki ya Mavazi ("Safari fashion week") Mkoani Manyara pamoja na kutembelea hifadhi ya utalii ya Manyara.
Akizungumza na Michuzi Blog, Mkurugenzi wa hoteli ya Mawemawe Caroline Ramoni amesema Nia yake thabiti ni kuwapa nafasi ya wabunifu kutembelea hifadhi ya utalii ya Manyara pamoja na Kuonyesha watanzania kuwa hata sehemu za hifadhi Kuna baadhi ya Mavazi huhitajika.
"Japo msukumo wa watanzania kutembelea hifadhi za utalii zilizopo nchini kwetu haujawa mkubwa sana lakini tumeonelea tuboreshe baadhi ya vitu ikiwemo kuwepo Kwa Mavazi ambayo yamebuniwa na wabunifu wetu na Mavazi hayo yatatumika pindi watalii watakapotembelea hifadhi hiyo."
Ramoni ameeleza kutokana na kuwepo Kwa changamoto ya ugonjwa wa uviko 19 biashara hiyo ya hoteli iliyopo mbugani Manyara haikuweza kupata wateja Kwa wingi kama ilivotegemewa hususani watalii kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa kutakua na muendelezo wa watu maarufu kutembelea hifadhi hiyo ya Manyara Ili kuona Kwa jinsi gani wanatangaza utalii.
Kwa upande wake Mratibu wa jukwaa hilo la ubunifu Lilian Massa amefafanua zaidi wabunifu ambao watashiriki katika Onyesho hilo la( "Safari fashion week" )ni pamoja na Ally Remtullah,Mustafa Hassanali, Jamila vera swai,Martin Kadinda,Doreen Mashika,Bahati Zanzibar, na wengine wengi.
Lengo la kuandaa Onyesho hilo likiwa ni kuwakutanisha pamoja wabunifu hao kufurahia vivutio vilivyopo nchini Huku wakipata nafasi ya kuuza nguo zao pamoja na mapambo ndani ya hifadhi hiyo ya Manyara.
Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika Januari 28 hadi 30, mwaka huu katika Hoteli ya Mawemawe mkoani Manyara na usahili wa kutafuta wanamitindo litafanyika mapema januari 15 katika ukumbi wa Makuti oysterbay jijini Dar es salaam.
Aidha, Onyesho hilo litawapa nafasi watu mbalimbali kuhudhuriwa Kwa kununua tiketi kwa kiingilio cha dola 50 Ili kuweza kushuhudia Kwa mara ya kwanza nguo ambazo zimetengenezwa Kwa ajili ya safari za kutalii hasa mbugani.
Miongoni mwa wabunifu watakaoshiriki katika Onyesho la "Safari fashion week" Mustafa Hassanali, Jamila vera swai na Martin Kadinda linalotarajiwa kufanyika januari 28 Hadi 30 mwaka huu katika hoteli ya Mawemawe iliyopo Manyara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...