Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya wanging’ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani humo kuwafanyia uchunguzi maafisa wawili wa ardhi akiwemo afisa ardhi msaidizi Cosmas Buja na mpima ardhi, Albert Mwakipesile kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kupokea rushwa.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wilayani humo, Kanoni amesema kuwa watumishi hao wamekuwa wakituhumiwa kupokea rushwa na kuruhusu wananchi kuendeleza maeneo ambayo hayatakiwi kisheria.
“Idara ya ardhi ina watumishi wachache lakini watumishi hawa ni kero,ni shida ni wabadhirifu na mambo mengine.Nimepokea malalamiko ya kila aina sasa imefika mwisho,nimetoa maelekezo kwa TAKUKURU kuanzia leo wachukue hatua”alisema Lauteri Kanoni “Kuna Buja ni shida sana huyu na kuna mwakipesil,hawa TAKUKURU fanyeni nao kazi na hadidu za rejea nitawapa mara moja kuanzia leo”aliongeza Kanoni
Aidha mkuu wa wilaya hiyo amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha shule zote za sekondari ambazo zilipokea fedha milioni 80 kwa kila shule kwaajili ya ujenzi wa mabweni, zinakamilisha ujenzi huo mwezi wa tatu mwaka huu.
Baadhi ya madiwani wamepokea kwa mtizamo chanya maagizo ya mkuu wa wilaya hiyo,huku wakiwataka wataalam kuwajibika kwa uadilifu katika nafasi zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...