Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Seleman Jafo ametoa maelekezo ya Serikali kila halmashauri nchini inatakiwa kupanda miti milioni 1.5 huku mkakati wa Serikali kwa nchi nzima ni kuhakikisha inapandwa miti milioni 276 kwa kila mwaka huku akitumia nafasi hiyo kulipongeza Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)kwa namna linavyosimamia vema sheria, sera na kanuni za utunzaji mazingira.
Pia Waziri Dk.Jafo ametoa pongezi kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Kamishna wa Uhifadhi Profesa Dos Santos Silayo na timu yake kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha maeneo yote ya uhifadhi yaendelea kutunzwa na kuboreshwa vema ili kuwa vivutio vya utalii huki akisisitiza maeneo yeto ya uhifadhi yaendelee kutunzwa na Watanzania wote.
Akizungumza leo Januari 11,mwaka 2022 baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi akiwa amepambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dk.Samweli Gwamaka pamoja na Kamishna Msaidizi wa TFS Kanda ya Mashariki Kamanda Carlorine Malundo, Waziri Jafo ametumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kupanda miti, hivyo amewataka Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kusimamia upandaji huo wa miti.
"Mchakato wa kupanda miti ulisuasua kwasababu ya ukame lakini sasa hivi mvua zimeanza kunyesha ,hivyo maelekezo ya ofisi yetu kila halmashauri ianze programu ya kutumia mvua hizi zinazonyesha kupanda miti ili kufikia lengo la kupanda miti milioni 276 na imani yangu wakuu wote wa mikoa na wilaya watasimamia katika mikoa yao, wilaya zao ajenda ya kupanda miti katika halmashauri , hili liende sambamba na kusimamia vitalu vya miti katika halmashauri.
"Tunajua kwa kila halmashauri imepewa muogozo wa uwekaji wa vitalu kwa lengo la kusaidia katika maeneo mbalimbali hasa ya taasisi za umma, tunataka kuona katika shule zetu zote , vituo vya afya na hospitali na maeneo yote ya taasisi za umma wanapandwa miti lakini ni vema wakachanganya na miti ya matunda.
"Binafsi nieleze tu Kamishna Msaidizi wa TFS nimefarijika sana kwa kazi ambayo mnaifanya katika kuendelea kuhifadhi maeno yote ya uhifadhi tukianza na hapa msitu wa Pugu ambao leo nimetembelea.Peleka salamu zangu kwa Kamishna wa Uhifadhi TFS Profesa Silayo kwamba anafanya kazi kubwa na nzuri sana, tunaomba maeneo yote ya misitu sasa yahifadhiwe vizuri,"amesema Waziri Jafo.
Ameongeza "Tumejisifu kule duniani kwamba sisi Tanzania tumehifadhi hekari milioni 48.1 lakini eneo la hifadhi zaidi ya asilimia 32 ya nchi yetu imehifadhiwa lakini kila mwaka tunapanda miti milioni 276 , ni ajenda ambayo duniani tunasifika, niowambe Watanzania tuendelee kulinda mazingira yetu".
Aidha amewaomba wananchi waache kuchoma miti na misitu hovyo na hiyo ndio isaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira."Nitume nafasi hii tena kuwapongeza NEMC kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusimamia sheria katika maeneo yote, niwaombe watanzania wote sasa tuwekeze katika utunzaji wa mazingira tukiangalia hali ya sasa kiwango cha joto hata hapa nchini kimeongezeka na imekuwa ikitishia maisha ya watu."
Waziri Dk.Jafo amesema kwa Tanzania wanamshukuru Rais kwa maelekezo yake kwani akiwa katika mikutano mbalimbali ajenda yake kubwa ni Watanzania wanapaswa kulinda na kuhifadhi mazingira yetu na yeye akiwa Waziri mwenye dhamana wakiongozwa na sera ya Mazingira ya mwaka 1997 ambayo ilifanyiwa marejeo mwaka 2021 pamoja na Sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 jukumu kubwa ni kuhakikisha wanaendelea kusimamia mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mku wa NEMC Dk.Samweli Gwamaka ametumia nafasi hiyo kwanza kumshuru Rais Samia Suluhu Hassan kwani katika hotuba zake zote neno mazingira halijakosekana na hii inaonesha ni jinsi gani ameweka mbele umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika nchini.
"Lakini nitoe shukrani nyingi kwa Waziri Dk.Jafo kwa kuchukua nafasi hii kuja Kisarawe , kuja kutembelea msitu huu wa Pugu kazimzumbwi na kushiriki katika upandaji miti ili Watanzania wote waweze kujua faida za mazingira jinsi ziliivyo.Ukija mahali hapa(Pugu)hutaki hata uondoke kwasaabu hali ya hewa ni safi.
"Mazingira ni safi lakini vile vile ukiangalia Ikolojia ilivyo iko kama vile ambavyo Mungu aliumba,sasa tunachotaka watanzania hebu tuhakikishe maeneo yetu yanarudi katika ualisia wake wa awali, kama alivyozungumza Waziri wetu kila familia ikipanda miti mitatu na ikatunza naamini Tanzania nzima itakuwa imejewa na misitu na tutapunguza athari ambazo tumekuwa tukizipata kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
"Kwa hiyo ninaomba na niwatake watanzania tunaendelea kushirikiana na kuhakikisha tunatunza mazingira kwani hili ni suala la maisha ya kwetu , mtu atakuwa bora pale mazingia tunayoishi yanakuwa bora kama tulivyoona katika msitu huu wa Pugu,"amesema Dk.Gwamaka.
Awali Kamishna Msaidizi wa TFS Kanda ya Mashariki Kamanda Carlorine Malundo amemueleza Waziri Jafo kuwa hifadhi ya msitu wa mazingira asilia Pugu kazi mzumbwi imetangwa kwenye tangazo la Serikali GN namba 190 ya Machi 6 mwaka 2020 wenye ukubwa wa hekta 8965 baada ya kupandishwa hadhi ya kuunganishwa kwa misitu ya uwanda wa Pwani(Msitu wa Pugu na Kazimzumbwi wilayani Kisarawe na Msitu wa Vikundu wilayani Mkuranga.
Kuhusu hal ya hifadhi ya msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Kamanda Malundo amesema kwa sasa hali ya uhifadhi inazidi kuimarika kutokana na tijitahada mbalimbali za uhifadhi zinazofanywa na TFS kwa kushirikia na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe pamoja na jamii zinazopakana na hifadhi hiyo.
Akizungumzia hali ya upandaji miti, amesem mwaka wa fedha wa 2020/2021 jumla ya miti 38520 imepandwa na kati ya hiyo miti 29750 ilipandwa maeneo yaliyoharibiwa katika msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi na miti 8770 ilipandwa katika maeneo ya taasisi na watu binafsi kwa kushrikiana a wadau wa mazingira wakiwemo WWF.
"Kwa mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 hadi sasa jumla ya miti 2430 imepandwa na miti 1130 imepandwa maeneo yaliyoharibiwa ndani ya msitu wa Pugu kazimzumbwi na miti 13000 imepandwa kwenye shule tatu za sekondari.Miche hii ya miti inazalishwa kwenye vitalu vya miti vya TFS,"amesema huki akifafana uboreshaji na uhamasisha wa utalii ikolojia umesababisha idadi ya watalii kuongezeka ndani ya msitu huo na kwa sehemu kubwa TFS wanamshukuru Jakate Mwegelo ambaye akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alifanya kazi kubwa kuhamasisha wananchi kutembelea msitu huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...