WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt, Ashatu Kijaji, amekutana na wawekezaji, na wamiliki wa viwanda mbalimbali  na kujadiili changamoto wanazokabiliana nazo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini na kujenga uchumi shindani na viwanda. 

Katika mikutano hiyo, Waziri Kijaji amekutana na Viongozi wa Kampuni ya Dangote Tanzania inayozalisha Saruji, Kampuni ya Coca - Cola Kwanza ltd inayozalisha bidhaa mbalimbali za vinywaji baridi na Wawekezaji wa Kampuni ya Gynile kutoka Misri inayotarajia kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mbolea nchini. 

Wakati huo huo, Waziri Kijaji amekutana na baadhi ya Watendaji na  Wakuu wa Tume ya Ushindani (FFC), Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB ) na  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na  Biashara kujadili utekelezaji wa  majukumu ya Taasisi hizo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kuleta maendeleo kwa taifa.

Aidha  Waziri Dkt. kijaji amezitaka taasisi zote chini ya Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara kufanya kazi kwa ushirikikiano na kuepuka kuwa kikwazo kwa wawekezaji, wenye viwanda na wafanyabiashara  ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ili kuendeleza na kukuza sekta ya uwekezaji, Viwanda na Biashara.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...